HALMASHAURI ya Wilaya ya Kibaha imepokea gari ya wagonjwa ambayo itatumika katika Hospitali ya Wilaya hiyo na kuondoa kero iliyokuwepo awali iliyosababishwa na uhaba wa magari hayo.

Kwasasa Halmashauri ya Wilaya Ina magari manne ya wagonjwa awali changamoto zaidi ilikuwa katika kituo cha afya Mlandizi ambacho kipo Mjini na kinahudumia wagonjwa wengi zaidi

Akikabidhi gari hilo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Michael Mwakamo alitaka gari hilo kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa Ili lidumu kwa muda mrefu.

Mwakamo aliwataka watendaji kutotumia gari hilo kama daladala kwa ajili ya kwenda kazini badala yake waendelee kutumia bajaji na usafiri mwingine.

"Gari hili linakuja kuondoa changamoto ya uhaba wa magari iliyokuwepo awali, litumike kwa malengo yaliyokusudiwa Ili kuendelea kuwasaidia wagonjwa," alisema.

Mwakamo alijivunia jitihada zake za kuleta maendeleo katika Jimbo hilo huku akiishukuru Serikali kwa namna inavyotoa fedha na vitendea kazi kumaliza kero za Wananchi.

Ametaka pia Wananchi kuwapima viongozi kwa kazi wanazofanya hususani za kuondoa vikwazo vya maendeleo kwenye maeneo yao kama inavyofanya Serikali ya awamu ya sita.

" Rais Dk.Samia Suluhu Hassan tunamshukuru kwa namna ambavyo ameendelea kubadilisha Jimbo letu kwa maendeleo kila sekta ameigusa anatufanya tujivunie kwa wananchi wetu " alieleza.

Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dk.Wilford Kondo alisema kwamba hakuna mgonjwa atakayetizwa fedha kwa huduma ya gari hilo la wagonjwa na kwamba atakayedaiwa fedha ya mafuta atoe taarifa.

Dk Kondo aliwataka Wananchi kufika kupata huduma katika Hospitali ya Wilaya kwani huduma nyingi kwasasa zinapatikana katika Hospitali hiyo tofauti na awali ambapo ilikuwa lazima mgonjwa apewe rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.

Diwani wa Mlandizi Euphrasia Kadala akiishukuru Serikali kwa kutoa gari hilo la wagonjwa kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ambalo sasa litakwenda kuondoa adha ya kukodi magari pindi lililopo linapopata hitilafu.

Tatu Haji na John Pilly ni wakazi wa Mlandizi ambao wanaishukuru Serikali kwa ajili ya gari hilo litakalosaidia kuhudumia wagonjwa kwa haraka.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...