Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga mapema leo ameongoza zoezi la upandaji wa miti lililoendana na ukataji wa keki kwa ajili kusherekea miaka 64 ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiongoza zoezi hilo la upandaji na kukata keki lililofanyika katika Shule ya Sekondari ya Katesh - Hanang, Mhe. Sendiga amesema Miti zaidi ya 3,000 imepandwa katika maeneo yaliyoathiriwa na maporomoko ya tope, mawe na magogo ikiwa ni njia mojawapo ya kurejesha uoto wa asili uliopotea kufuatia uharibifu mkubwa wa mazingira uliosababishwa na mafuriko yaliyotokea mwishoni mwaka mwaka jana.

Zoezi hilo lilihudhuriwa na Viongozi mbali mbali wakiwemo Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Wakuu wa Wilaya wote wa Mkoa wa Manyara, wananchi pamoja na watoto walioadhirika katika maporomoko hayo.

Mkoa wa Manyara umejipanga kupanda miti milioni 10 kwa mwaka 2024.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...