Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam, Geofrey Mkinga kifafanua jambo katika kikao cha kutoa taarifa kwa kamati ya Siasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam leo Januari 18, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akifungua kikao ca kuwasilisha taarifa za maendeleo ya Mradi inayotekelezwa na TARURA na TANROADS mkoa wa Dar es Salaam leo Januari 18, 2024.
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa DMDP, Nyariri Nanai akitoa taarifa katika kikao cha kamati ya siasa ya CCM mkoa wa Dar es Salaam.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam, Geofrey Mkinga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa taarifa ya Mradi wa DMDP awamu ya kwanza na awamu ya pili.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge akizungumza na waandishi wa habari jinsi alivyonufaika na Mradi wa DMDP awamu ya kwanza na namna atakavyonufaika katika maradi wa pili wa 2024.
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa DMDP, Nyariri Nanai akizungumza na waandishi wa habari.

VIONGOZI wa ngazi ya juu ya Chama Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, leo Januari 18, 2024 wamepokea taarifa ya Miradi ya maendeleo ya Mkoa, inayotekelezwa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD), inayoendelea kutekelezwa katika mkoa huo.

Miradi inayotekelezwa ni pamoja na mradi wa Bonde la Mto Msimbazi, Ujenzi wa Daraja la juu la jangwani, hali ya Barabara zilizoharibika kipindi cha Mvua na mpango wa Serikali katika karabati hizo.

Akitoa taarifaa katika kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Abas Mtemvu na kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Mratibu Msaidizi wa Mradi wa DMDP, Nyariri Nanai, amesema Dola za Kimarekani 438 zitatumika kati ya hizo ni Mkopo kutoka benki ya Dunia, fedha za ruzuku kutoka Serikali ya Uholanzi, zitakwenda kujenga barabara, kuboresha mifereji ya maji ya maji ya Mvua, kuboresha miundombinu ya umma kama Masoko na Stendinza mabasi, kusaidia eneo la taka ngumu na kuboresha madampo yaliyopo pamoja na kusafirisha taka kutoka katika madampo ya kisasa.

Amesema kuwa Miradi hiyo, mingi imekamilika kwa kiwango kikubwa cha utekelezaji wake katika awamu ya kwanza ambapo sasa mikakati kazi ya utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa DMDP unatarajiwa kuanza mwezi Mei 2024, ambao utajielekeza zaidi kwenye kujenga baadhi ya Barabara kuu na za mitaa katika Wilaya zote za jiji.

Aidha, kikao hicho pia kililenga kutatua kero zinazotokana na athari za mafuriko eneo la Jangwani, kulipa fidia Kwa waathirika wa mradi, kuzuia mmomonyoko, utunzaji wa maji, kurudisha uoto wa asili, kuweka mifumo ya kuruhusu maji kwenda baharini, kuweka mpango mji vizuri eneo hilo, kudhibiti athari ziyokanazo na taka ngumu pamoja na usimamizi wa bonde.

Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam, Geofrey Mkinga amesema kuwa Viongozi wa Chama kamati ya siasa mkoa wa Dar es Salaam walitaka kujua hatua mbalimbali zilipofikia katika Utekelezaji wa Mradi wa Bonde la Mto Msimbazi na Mradi wa DMDP awamu ya Pili.

"Tayari tumeshafikia hatua ya Usanifu wa barabara zitakazo kwenda kuanza kujengwa kwa awamu ya kwanza kwa mradi wa pili ambapo tunatarajia kuanza mwezi wa Pili kutangaza Zabuni ili Aprili na Mei wakandarasi wawepo katika maeneo ya kazi." Amesema Mkinga.

Akizungumzia bonde la Mto Msimbazi amesema hatua iliyofikiwa kwa awamu ya pili ya mradi ni kuanza kulipa fidia ili kupisha ujenzi wa daraja la juu katika mto huo ili TANROADS waingie kazini kuanzia Machi na Aprili wakandarasi wawepo Barabarani.

Kwa Upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge amesema kuwa hamashauri yake ni mnufaika wa miradi hiyo ya awamu ya kwanza na yapili jumla ya kilometa 48 zitakwenda kuwekwa lami katika manispaa hiyo kwa kuzingatia barabara zile zinazounganisha mitaa mbalimbali na zitakazounganisha kata na kata nyingine na barabara zinazounganisha manispaa ya Kinondoni na Manispaa nyingine zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam.




Ametolea mfano wa Barabara ambazo zimetengenezwa kwa Mradi wa DMDP wa awamu ya kuwa ni Barabara ya Tandale Msasani na Sinza.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa Mkuu wa Wenyeviti wa CCM wa Wilaya zote za Dar es Salaam, Makatibu wa CCM Wilaya, Mameya wa Wilaya, Mkurugenzi wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam, Mameya, Wataalamu na Mameneja Miradi wa TANROAD, wadau mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na Waandishi wa Habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...