BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Selemani Kidunda, amesema anajiandaa vyema kuhakikisha anashinda pambano lake dhidi ya Asemahle Wellem kutoka Afrika Kusini.

Kidunda atachapana na Wellem Machi Mosi mwaka huu katika pambano la raundi 10 la ubingwa wa WBF uzito wa juu, litakalofanyika Ukumbi wa Ubungo Plaza Machi 01,2024 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Michuziblog Kidunda amesema ameanza maandalizi mapema kumpiga mpinzani huyo na kuubakisha mkanda huo katika ardhi ya Tanzania.

“Watanzania watambue kuwa Wellem nitampiga kwa sababu mimi ni bondia ninayewapiga mabondia wagumu wote wanaokuja hapa nchini."

Mkanda huo hivi sasa unashikiliwa na Wellem aliyeshinda kwa kumpiga Mtanzania Twaha Kassim ‘Twaha Kiduku’, mwaka jana.

Kwa upande wake Mratibu wa pambano hilo "Kazi ngumu waachie wenyewe" Abdul amewaomba Mashabiki wa mchezo wa Masumbwi kujitokeza kwa wingi katika ukumbi wa Ubungo plaza mapema Machi 01,2024 kushuhudia burudani kutoka kwa mabondia wakali akiwemo Nasib Ramadhani maarufu "Packman ",Jesca Mfinanga akipambana na Lulu kayage huku pambano kubwa likisindikizwa na Seleman Kidunda "Jini Makata" dhidi ya Asemahle Wellem kutoka Afrika Kusini.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...