NAIBU Waziri wa Maji  Mhe.Mhandisi Maryprisca  Mahundi (Mb) amemuagiza Meneja wa Ruwasa wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Mhandisi Erwin Sizinga aweze kuhakikisha wanakamilisha ulazaji wa bomba wa umbali wa kilomita 2.8 ndani ya wiki moja ili wananchi wa Kata ya  Ubiri na Ngulwi waweze kupata huduma ya maji safi na salama.

Kadhalika  Mhandisi Mahundi amemuagiza Mkandarasi anayejenga Mradi wa Maji wa Magamba ahakikishe anaongeza kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ili aweze kukamilisha kwa wakati.

Mhandisi Mahundi ametoa maagizo hayo leo Januari 6  2024, alipotembelea na kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji ya Magamba na Mradi ya Maji Irente-Yoghoi-Ngulwi iliyopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

"Ili wananchi  elfu 30,835 wa maeneo ya Magamba, Kwesimu, Bara, Jegestal, Kambi namba nne, Chakechake, Kitivo, Maguzoni, Sinza, Lushoto Mjini, Mabwawani, Kipembe na Kialilo waweze kupata huduma ya maji miradi hii inapaswa kukamilika kwa wakati"amesema Mhandisi Mahundi

Naye  Mbunge wa Jimbo la Lushoto, Mhe. Shaban Shekilindi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutekeleza miradi ya maji kwenye jimbo hilo huku akisema  wananchi wengi watapata huduma ya maji huku akiwasisitiza wakandarasi kukamilisha kwa wakati.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...