Serikali ya awamu ya nane (8) imeimarisha Miundombinu ya Biashara, Afya, Elimu , Maji safi na salama, Mawasiliano na Uchukuzi ili kuendana na dhamira ya Mpinduzi Matukufu ya mwaka 1964 ya kuwaletea wananchi maendeleo, sambamba na kuimarishwa kwa dhana ya uchumi wa buluu ambayo ndio ajenda ya Kitaifa.

Akifungua kongamano la kuadhimisha miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar Mhe Hemed amesema malengo ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalilenga kuondoa ukoloni na kuimarisha uchumi na kuwaletea maendeleo wananchi hivyo Serikali inandelea kuimarisha miundombinu mbali mbali ambapo kwa upande wa Afya imefanikiwa kujenga hospitali kumi(10) za Wilaya na Hospital moja(1) ya Mkoa iliyoko Lumumba pamoja na kujenga na kukarabati vituo vya Afya vya msingi na ujenzi wa nyumba za mafaktari kwa Unguja na Pemba.

Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanikiwa kujenga shule sitini na nne(64)ambapo shule 34 ni za gorofa ikiwa lengo la Serikali ni kufikia azma ya wanafunzi kwenda shule kwa mkondo mmoja (1) kwa idadi ya wanafuzi arobaini na tano (45) kwa kila darasa.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali imeimarisha mazingira bora kwa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kwa kujenga masoko makubwa na yakisasa zyakiwemo soko la Mwanakwerekwe, Jumbi na Chuini kwa lengo la kuwawekea wafanya biasha mazingira mazuri wafanya biashara pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kuwapatia mikopo wajasiriamali ili waweze kujiendeleza kiuchumi.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha inayafanyia kazi mapendekezo na maazimio yatakayotolewa katika kongamano hilo ambayo yatasaidia katika kufikia maendeleo ya nchi pamoja na kuwataka wananchi kuendelea kuwa wasikivu na watulivu kwa kuipa ushirikiano Serikali yao inayoendelea kutekeleza mipango mizuri ya maendeleo.

Nae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe Tabia Maulid Mwita amesema malengo ya kufanyika kwa Mapinduzi Matukufu ya Mwaka 1964 ni kuimairisha uchumi wa Wazanzibari wazawa ambao wengi wao ni wakwezi na wakulima, kuimarisha amani na uzalendo kwa wananchi ambapo maono na falsafa zao zinaendelea kudumu na kuenziwa kwa maslahi ya Taifa .

Aidha amesema kuwa kufanyika kwa kongamano hilo kunatoa fursa kwa wale wote waliozaliwa baada ya mapinduzi kufahamu dhana nzima ya kufanyika kwa Mapinduzi ili kuweza kujua umuhimu wake na namna ya kuyalinda na kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Nao watoa mada katika kongamano hilo wamesema kuwa kufanyika kwa Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964 yalikuwa na lengo la kumkomboa Mzanzibari na mazila makubwa na utumwa waliofanyiwa na wakoloni kwa lengo la kujitawala na kufanya maamuzi yao wemyewe .

Wamesema kuwa mapinduzi ndio yaliyowajenga viongozi na wananchi kuwa wazalendo na nchi yao na kuwepo kwa Maendeleo, kuimarika kwa Amani na Utulivu, Upondo na mshikamano mambo ambayo hadi sasa yanazidi kuimarishwa na Serikali ya awamu ya nane (8) na kufikia ile dhamira ya waasisi wa Mapinduzi yaliyoongozwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Sheh Abeid Amani Karume.


Imetolewa na kitengo cha Habari (OMPR)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...