Mchana wa tarehe 31 Desemba 2023 kijijini Msoga wilaya ya Chalinze mkoani Pwani ukoo wa Kikwete walikuwa na sherehe kubwa ya jando na unyago.

Sherehe hiyo ilihusisha wavulana 11 na wasichana 7, wakiwemo watoto wa Mhe Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, na ndugu zake.

Wavulana na Wasichana hao waliotoka siku hiyo ni wajukuu wa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kaka zake na dada zake.

Sherehe hizo zilizofana sana kwa nyimbo na ngoma za kitamaduni zilifanyika baada ya vijana hao kumaliza takriban wiki mbili za mafunzo maalum kwenye kambi yao porini kwa mujibu wa mila na desturi za kabila la Wakwere.

Kwa mujibu wa wanakijijij wa Msoga waliohudhuria sherehe hizo, Wakwere bado wanaendeza mila ya jando na unyago kwa wavulana na wasichana wao ili kulinda na kudumisha kwa vitendo mila na desturi zinazohakikisha mtoto au kijana wao, kabla ya kuingia katika umri wa ki-utu uzima, anapata maarifa au stadi za maisha zinazomfanya awe kijana shupavu, anayejitambua na anayewajibika kikamilifu katika jamii na taifa. 

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa katika msherehe

Vijana wakitoka porini baada ya kuhitimu kambi ya mafunzo ya jando kijijini Msoga
Vijana wakitoka porini baada ya kuhitimu kambi ya mafunzo ya jando kijijini Msoga
 

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na kuratibiwa na Mhe Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa Chalinze ambaye pia ni Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakitembelea vijana kambini kwao usiku.

Vijana wakiwa tayari kuelekea kwenye sherehe za kuhitimu mafunzo ya Jando

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...