Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme la Tanzania,TANESCO Mha.Gissima Nyamo-hanga, ameelezea maendeleo ya TANESCO ndani ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar ,katika jukwaa la wakuu wa Taasisi lililofanyika Januari 13,2024 Unguja, Zanzibar

Katika jukwaa hilo Mha. Nyamo-hanga amesema kuwa kwa mara ya kwanza mwaka 1980 TANESCO ilijenga njia ya kusafirisha Umeme za ardhini zenye ukubwa wa kilometa 37.14 kutoka Rati kilomoni , Tegeta -Dar es salaam mpaka eneo la Rati Fumba - Zanzibar, kiasi cha Umeme wa Megawati 45.


“Miaka 43 iliyopita ambayo inakaribia na miaka 60 ya muungano wa Tanzania Bara na visiwani, Kwa mara ya kwanza tulijenga underground cable ya kusafirisha umeme kutoka Dar es salaam kuja zanzibar” alisema Mha. Nyamohanga

Aliongeza kwa kusema kuwa mwaka 2013 baada ya kuongezeka kwa matumizi ya umeme zanzibar, TANESCO ilijenga njia nyingine ya kusafirisha Umeme ya ardhini ya kuleta umeme Zanzibar iliyobeba umeme wa Megawati 100, njia hizo mbili ndizo zinazoendelea kutumika kuleta Umeme zanzibar hadi Sasa.

Akizungumzia Pemba,Mha.Nyamo-hanga amesema kuwa mwaka 2010 , Pemba iliunganishwa na Tanzania Bara kupitia Eneo la majani mapana Tanga, ambapo ilijengwa njia ya Umeme ya megawati 20, umbali wa kilometa78 chini ya bahari kufikisha Umeme Pemba, njia ambayo bado inaendelea kutumika kufikisha Umeme Pemba.

Aliongeza kwa kusema kuwa matumizi ya Zanzibar yanaongezeka siku hadi siku hivyo mpango uliowekwa na Shirika ni kujenga njia kubwa za Umeme zitakazokuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kusafirisha Umeme Zanzibar ili kuendana na mahitaji ya Umeme kwa Wananchi wa Unguja na Pemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...