Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wamekutana na kufanya kikao cha pili cha baraza la pili wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Erasmus Kipesha. Kikao hicho kilifanyika Januari 19, 2024 Mjini Morogoro.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao hicho Mwenyekiti wa Baraza hilo Dkt. Kipesha amesema, anawapongeza sana Sekretarieti ya Baraza kwa maandalizi mazuri ya kikao hicho muhimu kwa ajili ya kupitia na kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi na utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka.

Aidha, akiwasilisha taarifa ya Mamlaka kwa wajumbe wa Baraza hilo amesisitiza kuwa, ili TEA iweze kufikia malengo hasa ya kutekeleza miradi kwa ufanisi ni lazima utafutaji wa rasilimali upewe kipaombele na kila mtumishi.

"TEA ilianzishwa kwa sheria ya Mfuko wa Elimu na jukumu kuu la mfuko huo ni kutafuta rasilimali fedha kutoka kwa wadau mbalimbali wa masuala ya elimu ili kufadhili ujenzi wa miundombinu ya elimu", amesema Dkt. Kipesha

Ameongeza kuwa, utekelezaji wa jukumu hilo siyo wa mtu ama idara moja ndani ya mamlaka, bali ni wajibu wa kila mtumishi kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato ili kufikia malengo yaliyowekwa.

Wajumbe wa baraza walipokea taarifa hiyo ya Mkurugenzi Mkuu, wakaijadili na kuahidi kushirikiana kwa pamoja kutafuta wafadhili na wachangiaji wa elimu kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi alipokuwa akifungua kikao cha pili cha Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka hiyo mjini Morogoro

Mwakilishi kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya juu Tanzania (THTU) Taifa Bi. Salma Fundi, akiwasilisha salamu kutoka makao makuu ya chama hicho kwa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa TEA.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha akifafanua jambo katika kikao cha pili cha Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kilichofanyika mjini Morogoro.


Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la TEA wakisikiliza na kufuatilia taarifa mbalimbali zikiwasilishwa katika kikao cha pili cha Baraza hilo kilichofanyika mjini Morogoro.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha (Katikati) akisikiliza na kufuatilia taarifa mbalimbali katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika mjini Morogoro. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo kutoka  TEA Bw.Aidan Lucas   .

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka hiyo mjii Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...