Na; Mwandishi Wetu - Morogoro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameitaka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kuja na mfumo wa kidigitali ambao utarahisisha usuluhishi na utatuzi wa migogoro.

Prof. Ndalichako amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha tathimini ya utendaji kazi wa tume hiyo na mafunzo kilichofanyika leo tarehe 4 Januari, 2024 mkoani Morogoro.

Ameeleza kuwa, mfumo huo utasaidia kufanya utatuzi wenye haki na kwa wakati na pia kupunguza mrundikano wa kesi.

Kwa upande mwengine amewataka watumishi wa ofisi hiyo kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kwa bidii na waledi ili kuimarisha uchumi wa wananchi pamoja na taifa kwa ujumla.

Pia, amewasisitiza kila mtumishi katika ofisi hiyo kushiriki katika mafunzo hayo kwa kuwa yanalenga kuleta maendeleo na mahusiano mazuri katika utendaji kazi wao.

Naye, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose Mlyambina amesema Tume inatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na mahakama ili kuweza kupunguza mlundikano wa mashauri, kwani  Uchumi utakua kwa kasi na uwekezaji utaongezeka ukichochewa na huduma bora za utoaji haki hususani haki kazi.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Usekerege Mpulla amesema kuwa CMA itahakikisha ina anzisha mfumo wa kidijitali ambao utawawezesha watumishi kufuatilia taarifa na kurahisisha upatikanaji wa taarifa hizo.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...