Na Mwandishi Wetu

KESI inayowakabili Bharat Nathwani (57), maarufu kama Chiku na mkewe Sangita Bharat Nathwani (54) imepigwa kalenda hadi Februarri 19, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa dhidi ya mashitaka manne ikiwamo kujeruhi na kutoa lugha ya matusi.

Hatua hiyo ilifikiwa leo Januari 18, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa mshtakiwa anatuhumiwa na mashtaka manne, wanadaiwa kuyatenda Julai 21,2023 eneo la Mrima Kisutu, katika jengo la Lohana Wilaya ya Ilala alimjeruhi jirani yake.

Ilidaiwa kuwa Chiku baada ya kumjeruhi mke wa jirani yake, alisababishia madhara makubwa Kiran Lalit kwa kumzamisha kichwa chake kwenye ndoo ya saruji iliyomsababishia majeraha katika macho, masikio na kumsababishia maumivu shingoni.

Katika shitaka la pili la shambulio la mwili linalomkabili Chiku, siku ya tukio la kwanza na eneo hilo alimsababishia madhara kwa kumshambulia jirani yake Lalit Ratilal katika mwili wake kwa kumpiga ngumi na mateke kichwani.

Ilidaiwa kuwa katika shitaka la tatu na la nne linalomkabili Sangita, siku ya tukio alitoa lugha ya matusi dhidi ya majirani zake, Lalit na Kiran kitendo ambacho kilisababisha uvunjivu wa amani.

Wakili wa Serikali, Frank Michael akiomba ahirisho la kesi hiyo baada ya Hakimu Lyamuya kuwa na udhuru, Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga wa mahakama aliomba tarehe nyingine ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi wawili.


"Mheshimiwa tunao mashahidi wawili na tupo tayari kuendelea, lakini tulikuwa tunaomba tarehe nyingine ya usikilizwaji kwa sababu hakimu anayesikiliza kesi hii hayupo," alidai Wakili Michael.

Hakimu Kiswaga alisema kesi hiyo itasikilizwa Februari 19, mwaka huu na mashahidi hao wafike siku hiyo kutoa ushahidi wao.

" Mashahidi nawataka mfike tarehe hiyo na huyo shahidi ambaye amesema tarehe hiyo hatakuwepo atawasiliana na wakili wa serikali atatoa ushahidi wake kwa njia ya mtandao 'Video Conference' kwa sababu vifaa vipo," alisema Hakimu Kiswaga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...