Na Rahma Khamis. Maelezo. 3/1/224

Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Abeid Amani Karume amewataka Wananchi kuitunza, kuilinda amani na utulivu uliyopo nchini ili kuimarisha maendeleo.

Wito huo ameutoa huko Uroa Wilaya ya Kati wakati akifungua Hoteli ya YCONA ECO LUXURY RESORT, ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar.

Amesema bila amani na utulivu hakuna maendeleo yoyote yatakayopatikana hivyo ni vyema Wananchi kushirikiana na Viongozi wao katika kulinda na kudumisha amani na utulivu iliyopo nchini.

Amefahamisha kuwa kuwepo kwa amani na utulivu ni kichocheo cha Taifa lolote Duniani kupanga mipango ya Maendeleo na kuweza kuifanyia kazi.

"Tuendelee kuitunza amani na utulivu uliyopo kwa Umoja wetu na ushirikiano ili tuendelee kupata haya maendeleo tunayozungumza” alisisitiza Rais Mstaafu.

Amesema Mradi Hoteli hio ni wa kiasasa kwani umezingatia Mazingira yaliyopo hivyo utaleta Tija kubwa kwa Wananchi wa eneo hilo.

Aidha amewaasa wananchi kuacha tofauti za kisiasa na badala yake waendelea kushirikiana kwa maslahi yao na Taifa kwa Ujumla.

Akitoa maelezo ya Kitaalamu Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Sharif Ali Sharif amesema Mradi huo, utakapokamika utaekeza Dola Milioni 3 ambao ndio Mradi mkubwa kwa Zanzibar.

Amesema katika kipindi cha miaka mitatu ZIPA imetekeleza zaidi ya Miradi 200 na kuekeza zaidi ya Bilioni 14, Ajira laki 3 kwa Mkoa wa Kusini Unguja ambapo Ajira elfu tatu zimeshatolewa.

Aidh amefahamisha kuwa Jjumla ya Miradi 296 imeshatekelezwa na wanatarajia kujenga Hoteli kubwa ya nyota saba katika Kisiwa Cha Pemba na kukodisha Visiwa 16 ajili ya Uwekezaji.

Nae Meneja Muwekezaji wa Mradi huo Arnia amesema Mradi huo utawawezesha wazawa kupata Ajira na kuchangia kukuza Uwekezaji ili kuweza kuimarisha Uchumi wa Buluu.

Rais Mstaafu Awamu ya Sita Dk Amani Abeid Karume kulia akikunjuwa Kitambaa kuashiria  Ufunguzi wa  Hoteli ya Y-CONA Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

Rais Mstaafu Awamu ya Sita Dk Amani Abeid Karume akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika hafla ya Ufunguzi wa Hoteli ya Y-CONA Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
 

Rais Mstaafu Awamu ya Sita Dk Amani Abeid Karume akimsikiliza Mkurugenzi  Mtendaji wa ZIPA Sharif Ali Sharif wakati akitembelea  Hoteli ya Y-CONA katika hafla ya Ufunguzi wa Hoteli hio Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar .

Rais Mstaafu Awamu ya Sita Dk Amani Abeid Karume akikata Utepe  kuashiria  Ufunguzi wa  Hoteli ya Y-CONA Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Rais Mstaafu Awamu ya Sita Dk Amani Abeid Karume akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Ufunguzi wa  Hoteli ya Y-CONA  Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja .Ikiwa ni katika Shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...