Roma, 27 Januari 2024.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.), amewasili Roma, Italia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 - 29 Januari 2024, Roma, Italia.
Mara baada ya kuwasili, Waziri Makamba amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mohmoud Thabit Kombo.

Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo wa wangazi ya Wakuu wa Nchi wa Afrika na Italia, unatarajiwa kujadili ajenda mbalimbali zikijumuisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya miundombinu, ushirikishwaji wa wahamiaji katika kuleta maendeleo, usalama wa chakula, mapambano dhidi ya ugaidi na matumizi ya teknolojia ya kidigitali.

Ajenda nyingine ni pamoja na uhamiaji haramu, mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu, mabadiliko ya tabianchi, ushirikiano katika sekta ya elimu kupitia ngazi ya vyuo vikuu na katika mafunzo ya ufundi na utamaduni.

Kupitia mkutano huo Serikali ya Italia inatarajia kujipambanua kama mshirika muhimu wa maendeleo wa bara la Afrika kupitia mpango mpya wa maendeleo utakaotambulishwa kwa mara ya kwanza uitwao Mattei Plan. Mpango huo unalenga kuifanya Italia kushirikiana kwa karibu na bara la Afrika katika nyanja za maendeleo ya usawa na unatarajiwa kutambulishwa kwa nchi zingine za Umoja wa Ulaya hapo baadae utakapoanza utekelezaji. Vilevile kupitia Mkutano huo Italia inatarajia kutangaza kuunga mkono umuhimu wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika (AU) kuwa mwanachama kwenye Kundi la G-20.

Kadhalika, Italia inatarajia kutumia fursa ya mkutano huo, kuonesha utayari wake wa kuhamisha teknolojia ya kisasa (the know-how) katika sekta ya kilimo kwa nchi za Afrika na kuwa kitovu cha usambazaji wa Nishati kutoka Bara la Afrika.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...