WAF - Dar es Salaam

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeongeza kasi ya kutoa elimu na dawakinga kwa jamii ili kuyatokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ifikapo 2030.
Yameelezwa hayo na Afisa Programu kutoka Mpango wa Taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Wizara ya Afya Dkt. Isaac Njau katika semina ya kwa waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam niaba ya Meneja Mpango huo.

Amesema, mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele Duniani (matende na mabusha, Usubi, Trakoma, Kichocho na Minyoo ya tumbo) inayotarajiwa kufanyika Januari 30, mwaka huu.

“Mwaka huu tumejipanga kuadhimisha Siku ya Magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, maadhimisho yatafanyika ngazi za mikoa na halmashauri kwa kutoa elimu na hamasa juu ya magonjwa haya katika jamii." Amesema. 

Dkt. Clara Mwansasu ni Afisa kutoka Mpango huo wa kutokomeza magonjwa  yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ameeleza kuwa, Tanzania imekuwa ikitekeleza afua za kutokomeza magonjwa hayo ikiwemo kutoa elimu na kumezesha dawa (NTD’s) baada ya kuwa imefanya tathmini ya kina.

Sambamba na hilo, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushiriki katika utekelezaji wa afua nyinginezo ikiwamo usafi wa mazingira na mwili kwani ni moja ya visababishi vikubwa vya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...