Kituo cha kutoa huduma kwa wateja kilichoboreshwa zaidi cha Tigo-Zantel ambacho kitatoa huduma za kimataifa kimezinduliwa huko visiwani Zanzibar huku kikitarajiwa kumudu zaidi ya wateja millio1.5 waliopo katika visiwa hivyo ikiwemo visiwa vya Pemba.

Mwangaza Matotola mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja alisisitiza Shakira ya kampuni hiyo kuwa ni kuwafikia wateja wengi zaidi.

Uzinduzi huo unaashiria kufikia hatua muhimu katika visiwa vya Zanzibar ikiwa ni maendeleo makubwa ya mafanikio yaliyopatikana kwa muunganiko wa Tigo na Zantel ikiwemo uwekezaji uliofanyika kuhakikisha huduma zinaendelea kupatikana kwa kiwango cha juu kwa wateja.

Aidha Mwangaza aliongeza kuwa Kituo hichi cha huduma kwa wateja kimeimarishwa kutokana na kuwa na teknolojia ya kisasa ikiwemo kulinda taarifa za mteja kwa usalama wa hali ya juu.

Aliongeza kuwa Kwa ushirikiano wa mfumo wa USSD/SMS wa ufuatiliaji na upanuzi wa hoja, pamoja na ufuatiliaji wa 100% wa CRM wa kuridhisha wateja, huduma kwa wateja ya Tigo Zantel imepangwa kufikia watu wengi zaidi ikiwemo kufanya kazi muwda wote pia kituo hiki kitakuwa kikitoa huduma kila siku ili kuhakikisha tumchangamoto za wateja zinatatuliwa pamoja na kupunguza foleni zisizokuwa za lazima.

Vile vile alisema kuwa kituo kimeundwa kwa ufanisi mkubwa ikiwemo wateja kujibiwa maswali mbalimbali kwa ufasaha.

"Dhamira yetu ni kuhakikisha tunapanua njia za masiliano ambapo tayari tumeshawekeza zaidi ya sh. Trilioni moja tangu mwaka 2022 pia
Kituo cha huduma kwa wateja kilichoboreshwa ni mfano wa wazi wa ari hii, iliyoimarishwa na mawakala wa kitaalamu wa Kituo cha Simu, wakituweka katika nafasi nzuri ya kutoa huduma bora kwa wateja isiyo kifani. Mpango wetu wa kimkakati wa kuimarisha na kuboresha miundombinu ya mtandao wetu haujatuletea sifa tu ndani na kimataifa, ikiwa ni pamoja na tuzo ya kifahari ya OoklaSpeedtest lakini pia umeinua kwa kiasi kikubwa matumizi ya kidijitali kwa wateja wetu."

Katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar, Mahmoud Mohammed Musa, alipongeza kampuni hiyo kutokana na uwekezaji wake visiwani Zanzibar.

Alisema kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele kutoa huduma za kisasa visiwani humo ikiwemo Tigo Zantel kuongoza sokoni katika kutoa huduma bora kwa wateja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...