NA FARIDA MANGUBE MOROGORO

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imesema haitowavumilia na kufumbia macho viongozi walioshindwa kusimamia na kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule za awali, msingi na sekondari licha ya maelekezo ya Serikali ya kumaliza ujenzi Disemba 30, 2023.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Adolf Ndunguru wakati akifungua kikao kazi kwa Makatibu Tawala Wasaidizi Elimu na Maafisa Elimu wa Halmashauri zote nchini, na kuwataka kukamilisha miradi hiyo ifikapo Januari 15, 2024

Amesema Serikali imeendelea na utekelezaji wa maboreso ya sekta ya elimu ambapo Shilingi Tilioni 1.41zimekwishatengwa katika kipindi cha mwaka 2020/21 hadi 2023/24 kwajili ya ujezi wa miundombinu ya shule za awali, msingi na sekondari ikiwa ni moja ya hatua madhubuti zinazoendelea kutekelezwa.

Ameeleza kuwa baadhi ya Mikoa ujenzi wa miradi ya Shule upo chini ya 50% licha ya serikali kuelekeza miradi hiyo kukamilika kwa wakati uliopangwa, uzembe ambao kwa wale wanaosimamia miradi hiyo wanapaswa kujitafakari na kuachana na visingizio vya kutokamilisha kazi waliyokabidhiwa kuitekeleza.

“Nasikitika kusema pamoja na dhamira njema ya serikali kutekeleza miradi hiyo, bado miongoni mwenu wachache, kuna viongozi kabisa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo kwa muda ulioapangwa, licha ya maelekezo ya seraikali kumalisha ifikapo Disemba 30, 2023” Amesema Ndunguru

Aidha Ndunguru amewataka viongozi hao kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ufundishaji na ujifunzaji, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kinidhamu walimu wasiotekeleza wajibu wao, kuhakikisha wanafunzi wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza wanamdu stadi za lugha ya Kingereza ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa uapnde wake Mwenyekiti wa maafisa elimu Michael Ligala amesema kiini cha kutokukamilika kwa wakati miradi ya ujenzi wa miuondombinu ya shule ni usimamizi mbovu kwa baadhi yao, huku akiwasihi kwa watakao kumbana na vikwazo vya kutokamilisha miradi hiiyo muda mwingine ulioongezwa kutoa taarifa mapema iwezekananvyo.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...