Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafisa Wakuu wa Biashara (STO) wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) amezisisitiza Nchi wananchama wa Mkataba huo kushirikiana kwa usawa kurekebisha sera zinazowezesha kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi hizo.

Mwenyekiti huyo wa STO Dkt. Abdallah ameyasema hayo Januari 26, 2024 alipokuwa akifungua Mkutano wa 16 wa Kamati ya Maafisa Wakuu wa Biashara wa AfCFTA unaofanyika Durban, Afrika Kusini, kuanzia tarehe 26 hadi 29 Januari 2024 ukiongozwa na Tanzania, ambayo ni Mwenyekiti wa AfCFTA kwa mwaka huu 2024.

Akifungua Mkutano huo,  Dkt. Abdallah alisisitiza kuwa Sera hizo zinazotungwa zinapaswa  kuondoa vikwazo, kukuza ushirikishwaji na kuhakikisha kuwa faida za AfCFTA zinafika pembe zote za Bara la Afrika.

"AfCFTA inawakilisha ishara ya matumaini na fursa, inatufunza katika maono ya pamoja ya kukuza maendeleo endelevu kupitia biashara imara ya ndani ya Afrika." Amesema Dkt Abdallah.

Vilevile amebainisha kuwa Kamati hiyo ina jukumu muhimu katika kuonyesha ufanisi wa utekelezaji wa  malengo ya AfCFTA kwa kushiriki katika mazungumzo ya wazi yanayolenga yaliyo bora kwa Afrika kwa ujumla, badala ya nchi binafsi.

"Tunapofanya majadiliano ya kina, tuwe na mtazamo mpana wa Afrika, tukizidi nchi zetu binafsi, tukitambua kuwa kila uamuzi tunaoufanya una uwezo wa kuathiri maisha ya mamilioni ya watu. Ni jukumu letu la pamoja kuhakikisha kuwa athari hizi ni nzuri, za usawa, na endelevu". Alisisitiza Dkt. Abdallah.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (Usimamizi na Uchumi) Bw. Elijah Mwandumbya amesema Mkutanobhuo unalenga kutatua masuala ya kikodi ili kurahisisha biashara katika Bara la Afrika





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...