Na Brown Jonas – WUSM, Ivory Coast

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ametembelea Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Laurent Pokou uliopo jijini San Pedro nchini Ivory Coast ili kujifunza na kuona namna ambavyo nchi hiyo imefanya maandalizi ya uenyeji wa AFCON 2023 ikiwemo ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya mashindano hayo makubwa Afrika.


Mhe Ndumbaro amefanya ziara hiyo sanjari na kuhudhuria mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon2023) yanayoendelea nchini humo kama sehemu ya Tanzania kuendelea kujiandaa na uenyeji wa mashindano hayo mwaka 2027 kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.

Mhe. Dkt. Ndumbaro amesema aina ya uwanja aliouona unafaa pia katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo amesema Serikali mbali na kuendelea kujenga viwanja vya michezo Dodoma na Arusha inaendelea kukaribisha wadau wengine kuunga mkono juhudi hizo katika ujenzi wa miundombinu ya michezo katika mikoa mingine.

Katika ziara hiyo, Mhe. Dkt. Ndumbaro ameambatana na Kaimu Balozi wa Kituo cha Abuja anayehudumia pia nchi ya Ivory Coast Bi. Judika Nagunwa, Kaimu Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo Bw. Ally Mayay na maafisa wengine wa wizara.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...