Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) inawakaribisha wananchi wote katika Maonesho ya Biashara ikiwa ni Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba ili kupata elimu juu ya Fursa ya Usafiri wa Anga.

Lengo kubwa la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) ni kukitangaza chuo chake cha Usafiri wa Anga (CATC) ambacho miongoni mwa vyuo 6 vilivyoidhinishwa na kupata Ithibati ya ICAO kwa ajili ya kutoa mafunzo ya usalama wa usafiri wa anga kwenye ukanda huu wa Afrika ambapo vyuo vingine Barani Afrika ni Dakar - Senegal, Douala - Cameroon, Johannesburg - Afrika ya Kusini, Lagos - Nigeria, Nairobi - Kenya.

Chuo cha CATC kwa muda mrefu sasa kimekuwa kikipokea wanafunzi kutoka nchini Botswana, baadhi ya nchi nyingine ambazo zinaleta wanafunzi chuoni hapo ni pamoja na Rwanda, Burundi, Uganda, Eswatini, Kenya, Zambia, Guinea Conakry, Msumbiji, Somalia, Namibia, Lesotho na Malawi.

Maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Fumba, Zanzibar yalianza tarehe 07 na yanaendelea hadi Januari 19, 2024.
Ofisa Mwandamizi Mdhibiti na Mtoa Taarifa za Anga kutoka TCAA kituo cha Zanzibar Hemed Omar akitoa maelezo kwa wananchi wakiofika katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo pamoja na Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) katika Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar
Mkuu wa Kitengo cha huduma za Viwanja Vya Ndege kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Thamarat Abeid akitoa elimu kuhusu kozi zinazotolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...