Na Mwandishi Wetu

Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP Ltd) imetiliana sahihi na jamii za Wabarbaig katika kijiji cha Gorimba Wilayani Hanang kuchepusha bomba la mafuta ili kukwepa kaburi la mmoja wa viongozi wa kimila anayeheshimika wa jamii hiyo.

Hatau hii ni sehemu ya kuonyesha kujali mila na tamaduni za jamii za Kitanzania pamoja na kuheshimu haki za binadamu,

Kutokana na tathmini ya kina ya athari za haki za kibinadamu na mchakato wa utwaaji wa ardhi, EACOP imebaini makundi matatu ya kikabila yanayoishi pembezoni yanayojitambulisha kama wazawa, ambayo yameguswa na mradi huo.

Makundi haya ni pamoja na jamii za Kimasai, Wadatoga (Wataturu na Wabarabaig), na jamii za Waakie. EACOP imekuwa ikizishirikisha jamii hizi na viongozi wao wa kimila kwa miaka kadhaa kama sehemu ya dhamira yake ya kujenga uwezo, kudhibiti athari za mradi kwenye ardhi, utamaduni, na mila zao, na kuwapatia taarifa kuhusu utekelezaji wa mradi na kupokea maoni yao.

EACOP imesema itaendelea na dhamira yake ya kuheshimu mila na kuhakikisha usimamizi mzuri wa athari zozote kwa kuzingatia urithi wa kitamaduni wa jamii hizo. Mradi umekamilisha mikataba kadhaa na jamii zilizoaguswa na mradi, ikiwa ni pamoja na Mpango wa EACOP wa makundi ya kikabila yanayoishi pembezoni yanavyojitambulisha kama wazawa na kutia saini mikataba ya FPIC na jamii za Wataturu na Waakie.

Mchakato wa FPIC ni kipengele muhimu cha dhamira ya EACOP katika kuhakikisha inafikia viwango vya kimataifa vya ufadhili na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu, hasa Kiwango cha 7 cha Utendaji cha IFC kuhusu Wazawa.

Utiaji saini huu unaashiria Mkataba wa pili wa FPIC kati ya jamii za Wadatoga na EACOP, kufuatia kusainiwa kwa Mkataba wa FPIC na jamii ya Wataturu ya Kijiji cha Mwamayoka Machi 2023. Utiaji saini wa Mkataba wa FPIC na Wataturu ulisimamiwa na Wendy Brown, Meneja Mkuu wa EACOP Tanzania na Viongozi wa jamii ya Wataturu, wakishuhudiwa na wanajamii, wakishirikiana na AZAKI, Mshauri wa EACOP wa makundi ya kikabila yanayoishi Katika Mazingira Magumu yanavyojitambulisha kama Wazawa, pamoja na viongozi wa serikali ya wilaya ya Igunga.

Dkt. Elifuraha Laltaika, Mshauri wa EACOP kuhusu makundi ya kikabila yanayoishi pembezoni yanayojitambulisha kama wazawa, alisisitiza dhamira ya mradi katika kupunguza athari kupitia ushirikiano wenye tija. Alionyesha kufurahishwa na utayari wa EACOP wa kuepuka athari katika urithi muhimu wa kitamaduni wakati wowote kadri iwezekanavyo.

Dkt. Laltaika alisisitiza ushirikiano mkubwa ulioanza 2018 kwa mikutano ya robo mwaka na viongozi wa kimila na wanajamii inayoendelea tangu 2020. Mazungumzo haya yameongeza uelewa wa kina kuhusu athari za mradi kwa kila jamii, ikiwa ni pamoja na utambuzi wa maeneo ya kitamaduni na maeneo ya kiimani yanayoweza kuguswa na mradi.

EACOP pia imefanyakazi kwa kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali tatu zenye uzoefu - Timu ya Rasilimali ya Jumuiya ya Ujamaa (UCRT), jukwaa la asasi zisizo za kiserikali za wafugaji (PINGO's Forum), na shirika la maendeleo ya jamii ya wafugaji wa parakuiyo (PAICODEO) – ili kuwezesha utekelezaji wa mpango wa EACOP kwa makundi ya kikabila yanayoishi katika mazingira magumu yanayojitambulisha kama wazawa, haswa kupitia ushirikishwaji wa jamii, kujenga uwezo kuhusu michakato na athari za mradi, na kushughulikia maswali na madukuduku ya jamii.

Katika kipindi cha kutiwa saini kwa Mkataba wa FPIC mjini Hanang, mwakilishi wa Jukwaa la PINGOs Nailejileji Tipap aliipongeza mradi wa EACOP kwa kulinda maslahi ya Wazawa na kuheshimu utamaduni na mila zao. Alitambua kuwa EACOP na serikali wamezingatia umuhimu wa mtindo wa maisha na tamaduni za Wazawa wakati wa utekelezaji wa mradi wa EACOP.

Kiongozi wa jumuiya ya Wabarabaig, akitafakari kuhusu kutiwa saini kwa mkataba huu, alikiri wazi kwamba EACOP imeonesha kuelewa na kuheshimu utamaduni wao, hasa kwa kupunguza njia katika eneo hili ili kuepuka athari kwenye maeneo ya kitamaduni.

Kutiwa saini kwa Mkataba wa FPIC na jamii ya Wabarabaig kunaashiria kupiga hatua nyingine mbele ya EACOP kujizatiti katika utekelezaji wa mradi unaowajibika na unaoshirikisha, kuheshimu haki na urithi wa kitamaduni wa Wazawa

Viongozi wa kabila la Wabarbaig James Gejaru (kushoto) na Marko Gidumwa (kulia) wakisaini mkataba kuchepusha bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki linalopita katika kijiji cha Gorimba wilaya ya Hanang kukwepa kaburi la mmoja wa viongozi wa kimila wa kabila hilo. Anayeshuhudia kati kati ni Emil Msisiri ambaye ni mratibu wa mradi.


Baadhi ya viongozi wa kimila wa kabila la Wabarbaig pamoja na baadhi ya viongozi wa Bomba la Mafuta ghafi la Africa Mashariki wakisaini mkataba kuchepusha bomba la mafuta linalopita katika kijiji cha Gorimba wilaya ya Hanang kukwepa kaburi la mmoja wa viongozi wa kimila wa kabila hilo.


Baadhi ya viongozi wa kimila wa kabila la Wabarbaig pamoja na wbaadhi ya viongozi wa Bomba la Mafuta ghafi la Africa Mashariki wakionyesha mikataba waliyotiliana saini kuchepusha bomba la mafuta linalopita katika kijiji cha Gorimba kukwepa kaburi la mmoja wa viongozi wa kimila wa kabila hilo.

Baadhi ya watu jamii ya Barbaig wakipiga makofi wakati wa utilianaji sahihi kati ya jamii hiyo na  Bomba la Mafuta ghafi la Africa Mashariki  kuchepusha bomba la mafuta linalopita katika kijiji cha Gorimba wilaya ya Hanang kukwepa kaburi la mmoja wa viongozi wa kimila wa kabila hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...