Na Janeth Raphael - MichuziTv Dodoma

Wito umetolewa kwa Wauzaji wa bidhaa Nchini kuwa na Utamaduni wa kutoa Risiti na kwa Wanunuzi pia kuwa Utaratibu huo wa kudai Risiti pindi wafanyapo manunuzi kwani kinyume chake ni kuahirisha tatizo, kwani kwa kufanya hivyo kutakuwepo mizozo katika suala la ulipaji wa Kodi.

Wito huo kwa Wanunuzi na Wauzaji wa bidhaa umetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Lameck Nchemba mapema leo hii Jijini Dodoma, katika Uzinduzi wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ambayo imekuwa ni moja ya maono ya muda mrefu ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Samia Suluhu Hassan.

"Huku watu wanaouza bidhaa watoe risiti,na watu wanaonunua bidhaa wadai risiti yeyote ambaye ataacha kufanya hivyo anaahirisha tatizo tu lakini huko mbele atakutana na mkono wa Sheria,tusiahirishe tatizo tufuate Sheria ili tusiingie kwenye mizozo isiyostahili".

Sambamba na hayo Waziri Nchemba ameitaka Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kutofanya mzaha na wale wanaokiuka sheria,na kuhakikisha mtu analipa Kodi stahiki.

"Kwahiyo TRA Wala msifanye mchezo na mtu anayekiuka Sheria,mtun anayekiuka Sheria msifanye mchezo nae, Zingatieni Sheria,Zingatieni Weledi, Zingatieni mtu alipe Kodi stahiki msimbambikizie mtu Kodi alipe Kodi anayostahili".

Pia Waziri amesema kuwa Takwimu za walipa Kodi za Nchi yetu bado hazituweki pazuri na uwiani bado ni changamoto.

"Ukienda kwenye Takwimu za Nchi yetu za walipa Kodi,ukienda kwenye Takwimu zote hazituweki pazuri Sana,ukiangalia uwiano wa Kodi ukaweka kwenye lesho ya GDP ya pato letu uwiano bado uko chini".

Awali akitoa salami za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Rosemary Senyamule amesema kuwa kuanzishwa kwa Taasisi hii kutapunguza Malalamiko waliyokuwa wanayapata kutoka kwa wafanya biashara kwani wamepata pa kuyapeleka.

"Najua Taasisi hii itakuwa na mchango mkubwa wa kutupunguzia sisi kero ambazo tumekuwa tukizipokea kutoka kwa wafanya biashara,kwani wamepata mahali pa kuzipeleka".

Naye Msuluhishi Bwana Robert Manyama amesema mikakati ya kutoa elimu kwa Umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari itazingatiwa.

"Hivyo mikakati ya utiaji Elimu kwa Umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii utazingatiwa tukishirikiana na wadau wetu mbalimbali".

Kwa upande wake Mwenyekiti Kamati ya kudumu ya Bunge la Bajeti Mh Daniel Silo umuhimu wa uwepo wa uwazi katika utekelezaji wa majukumu ndani ya Taasisi hiyo Ila kupata mafanikio.

"Mimi niendelee kusisitiza suala la uwazi katika kutekeleza majukumu ndani ya Taasisi ili kupunguza Malalamiko yasiyo ya lazima".

Taasisi hii imekuwa ni hitajio kubwa la Nchi, kwa Watanzania na hata Serikali kwa ujumla chini ya Mh Dkt Samia Suluhu Hassan Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...