KITUO cha Uwekezaji (TIC) kimeendelea kuchanja mbuga katika maeneo mbalimbali kuendeleza kutoa hamasa na elimu kwa watanzania juu ya uwekezjai nchini.

Aidha ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya Kitaifa kuhamasisha Uwekezaji wa ndani iliyozinduliwa rasmi na Waziri Mkuu Mh. Kasim Majaliwa mnamo Septemba, 2023, ikiwapata watanzania kutumia fursa za uwekezaji kwa kupewa kipaumbele kwa watanzania

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mipango Utafiti na Mifumo ya Computer Bw.Revocatus Rasheli akiwa katika mkoa wa Morogoro ameeleza faida na umuhimu wa mwekezaji mzawa yaani Mtanzania kusajili mradi wake katika kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC).

Rasheli pia ametembelea miradi iliyipo mkoani humo inayohusu utengenezaji wa chakula cha wanyama, kinachofahamika kama International Tranfeed Limited na Mkulanzi kiwanda cha sukari kilichopo Kilosa - dakawa
 

Mkurugenzi wa Mipango Utafiti na Mifumo ya Computer kutoka Kituo cha Uwekezaji (TIC) Revocatus Rasheli akizungumza na Wanahabari Faida na umuhimu wa mwekezaji mzawa kusajili mradi wake katika kituo hicho wakati alipotembelea miradi mbalimbali Mkoa wa Morogoro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...