WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, leo Januari 15, 2024 ameongoza kikao cha kwanza cha kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip, Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulah ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida pamoja na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...