NA BALTAZAR MASHAKA, MISUNGWI


WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) wamesema CCM imefanya mengi ya maendeleo ya kujivunia katika kipindi cha miaka 47 na kukifanya kiendelee kuaminika kwa wananchi na kushika dola.

Pia Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanyia wananchi mambo mengi mazuri ya maendeleo, hivyo hawana cha kumlipa zaidi ya kuchagua viongozi wazuri kutoka ndani ya CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo na na wajumbe wa NEC,Habiba Ali Mohamed (WAZAZI-Zanzibar) na Jamal Abdul ‘Babu’ mjumbe wa NEC Mkoa wa Mwanza, walipozungumza na wananchi wakiwemo wana CCM wa Wilaya ya Misungwi,katika maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama hicho.

“Niaombe wananchi wa Misungwi,uongozi wa Chama na Serikali chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,ametekeleza ilani ipasavyo,ametufanyia mengi mazuri na sote tunajionea miaka 47 sekta za afya,elimu,kilimo,maji na miundombinu ya barabara amefanya ka asilimia 100, tumuunge mkono,”amesema Habiba.

Amesema Mama Samia ametufanyia mambo mengi ambayo hatuna cha kumlipa, hivyo utakapofika uchaguzi wa serikali za mitaa katika vijiji na vitongoji msifanye makosa kura zote ziende kwa CCM,tumfurahishe Mama kwani ametufurahisha sana na katika uchaguzi wa 2025 tumpe mitano tena Kazi Iendelee.

Kwa upande wa Jamal amesema kazi nzuri iliyofanywa na CCM kwa miaka 47 inakifanya kiendelee kuaminika kwa wananchi na kushika dola,hakuna namna ya kukishinda katika uchaguzi mbalimbali.

“Miaka 47 kazi nzuri zimefanyika, wakati kinaanzishwa kilikuwa na vipaumbe vitatu vya kupigana na maradhi, ujinga na umasikini,kimeyafanya hayo na kusimamia demokrasia,hivyo tujipongeze kwa kushiriki kukikifikisha kilipofika bila kuwasahau Mwl Hayati Nyerere, Mwinyi,Ben Mkapa (Hayati),Jakaya Kikwete, Hayati Dk. Magufuli na sasa Dk.Samia,”amesema.

Mjumbe huyo wa NEC amesema leo chini ya mwanamke shupavu Dk.Samia CCM imeendelea kuimarika katika chaguzi kikitoka kuongoza wananchi milioni 17 na wanachama 500,000 mwaka 1977 , kimeendelea kuongoza Watanzania zaidi ya milioni 61.Pia amefanya mabadiliko makubwa ya kadi za kielektroniki na kuwezesha wana CCM kutambuliwa na mfumo na hivyo sifa ya CCM haiwezi kutenganisha na serikali ambapo ilianzisha shule kupamnana na ujinga, zahanati na hospitali (maradhi) na shughuli nyingine za uzalishaji kiuchumi kukabiliana na umasikini.

“Asiye shukuru watu hata Mungu hawezi kumsukuru, nawashukuru kwa kuja kuhudhuria miaka 47 ya kuzaliwa CCM.Misungwi kilio kikubwa kilikuwa maji ili hali Ziwa Victoria liko karibu,mbunge wa zamani wa hapa (Kitwanga au Mawe Matatu) alifikia uamuzi wa kusema ‘tutalala barabarani na wananchi wangu tukanyagwe na magari serikali isipoleta maji,”amesema Jamal.

Ameleza kuwa Rais Samia ameleta fedha sh. billion 38 za maji na anajenga mtandao wa matenki ya kuhifadhi lita milioni 3.5 yatakayohudumia kata tano ikiwemo Usagara,ameleta zaidi ya bilioni 77 za mradi wa maji Mbarika na Misasi na anajenga km 139 za barabara ya lami.

Amewataka madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa waliopo madarakani,waachwe wachape kazi na kuonya watu wenye chokochoko wanaotengeneza majungu dhidi ya wenzao na kuwapa matope.

“Wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kunakuwa na maneno maneno ya kuwatengenezea wenzenu ajali na majungu.Utasimama vipi kumnadi wakati ulimchafua? Hatutaki mpasuko, nafsi ya mwenyekiti wa CCM Wilaya Misungwi tutampata,”alisema Jamal.

Ameonya wanaochafua wana CCM wenzao na wenye makundi wakubali kuyavunja pindi wagombea wao wakishindwa katika sanduku la kura lakini kabla wagombea wote watatendewa haki na kusisitiza kuwa kasi iongezwe ya kuyasema yaliyofanywa na serikali huku akiwataka madiwani kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ili penye kasoro parekebishwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...