NA BALTAZAR MASHAKA,ILEMELA

MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,wamepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/25 ya sh. bilioni 81.458.

Hayo yameelezwa leo na Mchumi wa Manispaa ya Ilemela,Helbert Bilia kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo,Wakili Kiomoni Kibamba,katika kikao cha Bajeti cha Baraza la Madiwani.

Akiwasilisha Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mpango wa Bajeti ya mwaka 2024/25,Bilia amesema halmashauri inaomba kuidhinishiwa sh.bilioni 81.458 kati hizo sh. bilioni 10.067 ni ruzuku ya miradi ya maendeleo, sh.bilioni 14.774 ni mapato ya ndani ambapo kati ya hizo fedha sh. bilioni 8.068 ni za miradi ya maaendeleo.

Aidha sh. bilioni 55,611 ni mishahara ambayo imeongeka kutoka sh. bilioni 43.5 mwaka 2023/24 sababu ya ajira mpya, upandishaji wa madaraja an vyeo kwa watumishi mbalimbali,sh.bilioni 5.378 ni matumizi ya kawaida sh.bilioni 1.0 ni ruzuku ya matumizi mengineyo ya kawaida na sh.bilioni 1.327 za mapato fungwa.

“Mapendekezo haya yameandaliwa kwa kuzingatia Sheria ya Bajeti namba 11 ya mwaka 2015 na kuzingatia masuala ya Mpango wa Maendeleo wa Pili wa Miaka Mitano wa mwaka 2021/2022- 2025/2026, na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025,”alieleza Bilia na kuongeza;

“Pia Hotuba ya Mhe. Rais wa Awamu ya Sita wakati wa kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) 2020-2025,Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 -2025; Maelekezo ya Kamati za Kudumu za Halmashauri,Mwongozo wa Bajeti uliotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango wa mwaka wa fedha 2024/2025,maelekezo na ushauri wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza”.

Amefafanua kuwa Makisio ya Mapato hayo ya sh.bilioni 14.774 yanayotokana na vyanzo vya ndani kwa mwaka na kuainisha vipaumbele vya bajeti hiyo kuwa imejikita kutatua changamoto za sekta za elimu,afya,miundombinu na huduma za jamii.

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri hiyo ya Ilemela, Mwevi Ramadhani,Dede Swila,Rosemary Mayunga,Sarah Ng’wani, Jonathan Mkumba na Donald Ndaro wakichangia makadirio ya bajeti hiyo waliunga mkono kuwa inakwenda kujibu kero na changamoto za jamii kwa kiwango kikubwa ambapo baraza hilo la madiwani lilipitisha makadirio hayo kwa kishindo.

Akizungumzia mapitio ya bajeti ya mwaka 2023/24,Bilia amesema mapato na matumizi kwa kipindi kilichoishia Disemba, halmashauri ilipanga kukusanya na kutumia sh.bilioni 70.489 za shughuli za maendeleo na matumizi ya kawaida.

Amesema hadi kufikia Disemba 31, 2023 sh.bilioni 35.631 zilikusanywa kutoka vyanzo mbalimbali sawa na asilimia 51 ya lengo la bilioni 70.489 ambapo ruzuku ya maendeleo sh.bilioni 4.795 kati ya sh.bilioni 11.028,mapato ya ndani bilioni 7.146 kati ya lengo la sh. bilioni 14.876 na matumizi ya kawaida sh.milioni 579.52 kati ya bilioni 1.0.

“Halmashauri ilipanga kutumia sh.bilioni 35.631 kutekeleza miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2023/2024,hadi Disemba 31, 2023 sh.bilioni 33.104 zilitumika kutoka vyanzo mbalimbali hii ni sawa na asilimia 93 ya lengo,”amesema

Bilia amesema kutokana na utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2023/2024 (Julai – Desemba, 2023) hamlashauri ilikamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu tisa ya vyoo katika shule ya Sekondari Bwiru Wasichana kwa fedha za EP4R.

Pia imelipa fidia sh.bilioni 1.301 kwa wananchi waliopisha maeneo yao kwa ajili ya mradi wa upimaji eneo la Nyafula,barabara za Buswelu– Nyamadoke chini ya mradi wa TACTIC, pamoja na taasisi za umma zikiwemo shule.

Aidha halmashauri imekamilisha ujenzi wa shule mbili za msingi mpya (Busenga na Buteja) zenye mikondo miwili kwa fedha za Mradi wa BOOST,imekamilisha madarasa 16 na matundu 12 ya vyoo katika shule za Msingi Igombe, Nyamadoke, Nyamhongolo na Nyamwilolelwa kwa fedha za BOOST.

“Ujenzi wa madarasa manne (4 ) ya mfano ya shule ya awali katika shule ya Msingi Chasubi (2) na Nyamhongolo (2) kwa fedha za BOOST,shule mpya ya Sekondari Kisenga pia imekamilika kw fedha za mradi wa SEQUIP na tayari imesajiliwa na kupokea wanafunzi 309 wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2024,”ameeleza Bilia

Mchumi huyo amesema kupitia mradi wa TACTIC halmashauri imeanza utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Buswelu-Nyamadoke-Nyamhongolo, Buswelu-Busenga na Cocacola yenye urefu wa kilomita 12.8 kwa kiwango cha lami.

Amesema licha ya mafanikio katika baadhi ya maeneo, halmashauri bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za wananchi kutochangia miradi ya maendeleo inayoibuliwa na kushauri ufanyike uhamasishaji.

“Kuwepo miradi mingi ya jamii inayohitaji mchango wa halmashauri,inaendelea kuelimisha wananchi umuhimu wa kuchangia miradi ya maendeleo hususani mfumo wa O&OD ulioboreshwa,” amesema Bilia.

Changamoto nyingine ni uhaba wa magari ya uzoaji taka na taratibu za manunuzi ya mitambo ya taka ngumu,uongozi umeanza kukabiliana na tatizo hilo,uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ambapo mahitaji ni walimu 510 na waliopo ni 264, hivyo maombi maalum yamewasilishwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kupata ajira mpya kwa walimu wa sayansi tu

Mchumi na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela,Herbert Bilia Akiwasilisha Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mpango na Bajeti ya mwak 2024/25 katika Baraza la Madiwani wa Manipaa hiyo leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...