NA WILLIUM PAUL, SAME.

KATIBU wa Nec, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kupitia Chama cha Mapinduzi (SUKI), Rabia Abdallah Hamid amewataka wanachama wa chama hicho kuepuka makundi kipindi hiki ambacho wanaelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu 2025.

Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya CCM (MCC) alitoa kauli hiyo jana wakati alipozungumza na wanachama wa CCM wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro ikiwa ni maadhimisho ya miaka 47 tangu kuzaliwa kwa CCM.

Alisema kuwa, wapo baadhi ya wanachama ambao sio waaminifu wamekuwa wakieneza makundi kwa uchu wa madaraka na maslahi yao binafsi na kuwaonya kuwacha tabia hiyo huku akiwataka wanachama kutowaunga mkono.

"Kwa sasa chama kinamadiwani, Wabunge na Rais sasa hao waopita kujitangaza na kuanza kampeni kabla ya muda wanataka kutuharibia chama chetu na kututengenezea makundi tunapaswa kuwakataa maana sio watu wazuri kwa maslahi ya chama chetu" Alisema Rabia.

Katibu huyo wa SUKI alisema kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani imefanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi maendeleo ambapo imetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kuwataka wanaccm kuisemea miradi hiyo kwa wananchi ili waelewe.

Alisema kuwa, wapo baadhi ya watu kazi yao ni kueneza propaganda chafu mitandaoni na kuikashifu serikali kwa maneno ya uongo na kuwataka wanaccm kutoka na kujibu propaganda hizo.

Aidha alisema kuwa, katika kipindi chake cha ulezi mkoa wa Kilimanjaro atahakikisha anakuwa karibu na wanachama pamoja na wananchi na kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi aliahidi chama hicho kushinda viti vyote katika chaguzi za serikali za mitaa kutokana na kazi kubwa zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...