Na.Vero Ignatus,Arusha.
 
Kipindi cha Rika balehe kwa watoto ni wakati ambapo watoto hupatwa na wasiwasi   kutokana na  mabadiliko mengi katika miili yao,  ambapo mabadiliko haya hutokana na homoni ambazo husababisha mabadiliko kimwili,kiakili,kisaikolojia,kihisia,mahusiano yake na jamii,kibaiolojia na wakati huu ndipo  wengi wao  hujihusisha na tabia zisizofaa na hata kukutana na vishawishi kutoka kwa makundi rika.

Kipindi hichi ndicho  kile ambacho watoto wanajali muonekano wao kwa nje zaidi, anakuwa na maswali mwengi ambapo mzazi,mlezi ndipo unapotakiwa kutumia fursa hiyo kumpa ukweli juu ya maadili,Mabadiliko juu ya mwili wake   ,haiba mtazamo halisi juu ya muonekano wake mahusiano,hapa ndipo mzazi unatakiwa kuweka jitihada za kupanga na kutaka  kuwafahamu marafiki wa mtoto wako kwa karibu  hisia

"Kipindi hiki ndicho ambapo  anaweza kupata shinikizo rika kutumia pombe sigara shisha dawa za kulevya na hata kufanya ngono,changamoto nyingine zianweza kuwa kkupata msongo wa mawazo,ambapo katika umri huu watoto hufanya maamuzi wenyewe kuhusu marafiki michezo wanayoipenda na wakati huu ndio wanaona kuwa wanao uwezo wa kujitegemea japokuwa wanahitaji uangalizi wa wazazi kwa karibu''.  
Sospeter Bulugu  ni mwenyekiti wa mashujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania amesema kuwa zipo changamoto zinazopelekea mzazi kukosa msimamo wa kusimamia  watoto ikwemo hali ya duni katika familia kiuchumi kumudu gharama za masomo ,migogoro ya kifamilia kama vile wazazi kutengana (watoto kukosa msimamizi wa malezi wa tabia zao au mabadiliko yao ya kimwili na kimtazamo katika umri wa balehe.

Bulugu anasema kuwa malezi ndiyo hutafsiri malezi ya mwisho ya mtoto ,ikiwa ni maandalizi na usimamizi wa katika ukuaji wa mtoto,ukizingatia kuwa mtoto anatakiwa kupita katika mfumo wa shule kuanzia awali,msingi,sekondari( rika balehe) hadi chuo kikuu.

Amesisitiza kuwa Ukiona kuna pahala mtoto analegelega kutimiza malengo yake ya kuendelea na masomo mara nyingi inachangiwa na wazazi kutokuwa na msimamo juu ya tabia za mtoto ambazo katika rika balehe ni za kujaribu mambo mengi ambapo asipokanywa huwa zinageuka kuwa tabia na mitizamo ya moja kwa moja ambayo hupoteza muelekeo wa mtoto husika
Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum june 26, 2023 kupitia Naibu waziri Mwanaid Ali Khamis alifungua mafunzo ya kimataifa ya Sayansi na malezi,Makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwa wadau kutoka mikoa 16 nchini pamoja na wizara za kisekta mkoani Dodoma, lengo likiwa kuwaongezea ujuzi,lakini pia kuhakikisha kuwa wananchi kwani elimu ya malezi ni ya muhimu sana katika makuzi mtoto.

Aidha katika mafunzo hayo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia ,wanawake na Makundi maalum,Sebastian Kituku aliweza kusema kuwa wizara itaendelea kushirikiana vyema na wadau wa malezi ,makuzi na maendeleo ya mtoto ili kuhakikisha kuwa mazingira salama ya ustawi wa Maendeleo ya Mtoto nchini.

Hivyo basi Kutokana na  familia na jamii kupotoka na kuacha kufuata maadili mila na tamaduni za mtanzania Wizara ya maendeleo Jamii jinsia wanawake na makundi maalum kwa kushirikiana na Wizara ya habari mawasiliano na teknolojia kwa kupitia Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA ,zimejipanga kuanzia februari 2024 zimejipanga kuleta katika jamii  vipindi maalum  kwaajili ya kuelimisha umma juu  ya malezi ma makuzi ya mtoto pamoja na elimu  maadili kwa kijana lengo kubwa likiwa ni kupambana na mmomonyoko wa maadili unaoendelea hivi sasa  

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Michuzi Blog Wadau wa maendeleo kutoka Taasisi tofauti zisizo za kiserikali wamesema kuwa ifike wakati  jamii itambue  na kuwa  makini na malezi ya watoto wa kiume wanaoingia kwenye jukumu la kuitwa baba kabla ya wakati wake badala ya kuwatupia lawama na kusababisha kujiingiza kwenye makundi mengine yasiyostahili.

Aidha akifafanua juu ya suala la Watoto wa kiume wanaoingia kwenye majukumu ya kuitwa baba wakiwa na umri mdogo  mkurugenzi wa Vuka Inititative bi Veronica Ignatus Ignatus amesema: kuwa ni kweli kabisa kwamba jamii imesahau juu ya watoto wa kiume haswa wale wanaongia kwenye majukumu hayo wakiwa bado hawatambui nini cha kufanya kutokana na umri wao kuwa mdogo na bado wakiwa wanahitaji msaada kutoka kwa wazazi na walezi hadi pale watakapojitambua na kujisimamia wenyewe
 
"Sisi kama kama wazazi na walezi hata jamii kwa ujumla tumekuwa na kasumba ya kurusha lawama kwa watoto hawa wa kiume ,wanapofikia umri balehe kuna kuwa na mabadiliko mengi katika umri wao wa kutaka kujaribu kila jambo hapo ndipo  linapompelekea kujiingiza kwenye changamoto ya kuingia kwenye majukumu ya kuitwa baba kabla ya umri wake
.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...