Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani ,Mwinshehe Mlao, ametoa rai kwa wanachama wa CCM kutokisusa chama hicho pindi wanapokosa nafasi za uongozi wakati wa chaguzi mbalimbali.

Aliyasema hayo katika ziara ya kamati ya siasa Tarafa kwa Tarafa katika mkutano wa viongozi, wanachama na wananchi uliofanyika katika Kata ya Kirongwe Wilaya ya Mafia.

Mlao ameeleza, kila mwanaccm ana wajibu wa kuhakikisha CCM inapata ushindi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijijini na Vitongoji na si vinginevyo.

Aidha amesema wanachama wanapaswa kufanya kazi ya ziada ya kuwashawishi wasio wanachama kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi wakati na baada ya uchaguzi.

Mlao pia aliwataka wenye sifa za kugombea kujitokeza kugombea kwenye chaguzi zinazokuja kwani kila mmoja ana haki ya kugombea.

Wakati huo huo ,CCM wilaya Kibaha Mjini kinawatangazia wanachama wa CCM na wananchi wote wa Kibaha Mjini kwamba tarehe 09 Februari , Ijumaa kutakuwa na ziara ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao kuzungumza na wananchi kwa kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Mkutano wa hadhara utatanguliwa na kikao cha CCM cha ndani ukumbi wa Williams, ikiwajumuisha Halmashauri kuu CCM Wilaya Kibaha Mjini, Kamati za utekelezaji jumuiya zote 3 na mabaraza yote wilaya Kibaha Mjini ,kamati za Siasa za kata zote 14 viongozi wa dini na wazee.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...