VICTOR MASANGU,KIBAHA

 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM)  Mkoa wa  Pwani amewaonya vikali  baadhi ya wanachama  wa chama  na baadhi ya  wananchi wa mkoani Pwani  ambao wamekuwa na mazoea ya kuwatukana Viongozi wa Chama hicho kwenye mitandao ya kijamii kuacha mara moja.

Mlao ametoa onyo hilo Wilayani Kibaha wakati akizungumza na wananchi  pamoja na wana chama wa CCM   wakati wa ziara yake ya kawaida ya kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

Kwa upande wake katibu wa  chama cha mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Pwani Brnard Ghaty amewataka viongozi kuachana na tabia ya kutoa siri ya vikao mbali mbali ambavyo vinafanyika.

"Kuna baadhi ya watu tumeajiri lakini wamekuwa na changamoto ya kuamua kutoa siri za ndani ya vikao kwa kweli hii sio sahii kabisa kwa hiyo hii tabia tuachane nayo,"alifafanua Katibu.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa UWT  Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu  aliwataka Wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi huku Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka akieleza utekelezaji wa ilani

Naye Mwenyekiti wa wazazi Mkoa wa Pwani Jackson Kituka  amewahimiza viongozi kuhakikisha kwamba wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwatembelea wanachama.

Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma nyamka alisema kwamba utekelezaji wa ilani unaendelea kwa vitendo ikiwemo katika sekta ya afya elimu,maji pamoja na mambo mengine ya msingi.

"Kwa kweli utekelezaji wa ilani ya chama katika Wilaya yetu ya Kibaha kwa kweli unafanyika na ukiangalia miradi mbali mbali imetekelezwa hivyo ushahidi upo na siku zote mwenye macho aambiwi tazama,"alisema Nyamka.

Awali baadhi ya wana chama wa CCM na wananchi walieleza kero Mbalimbali zinazowakabili katika mitaa yao ikiwemo katika sekta ya miundombinu ya barabara,afya,maji pamoja na sekta ya elimu.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...