KWA mujibu wa utafiti wa masoko uliofanywa na -OMDIA imeitaja kampuni ya Samsung electronics Tanzania kukua kwa asilimia 30.1 kwa uuzwaji wa runinga katika soko la kimataifa kwa mwaka 2023.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu wa Samsung Electronics Tanzania Manish Jangra huku mafanikio hayo yakichangiwa na mikakati iliyoweka na kampuni hiyo katika kuleta runinga hizo kwa watanzania.

Amesema kampuni hiyo imevuka mauzo ya jumla na kufikia runinga milioni 40 huku safu ya runinga za QLED kwa mwaka jana pekee yalifikia mauzo milioni 8.31.

Tangu kuzinduliwa kwake 2017 kampuni hiyo kupitia bidhaa zake imeonekana kuchangia pato la Taifa hasa katika ulipaji kodi.

Aidha katika kuadhimisha mfululizo wa miaka 18 ya kampuni hiyo imeendelea kuleta vifaa bunifu ikiwemo runinga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...