Na. Peter Haule, WF, Dodoma

 

Serikali imesema kuwa imelipa jumla ya Shilingi trilioni 1.03 kati ya shilingi trilioni 1.41 za madeni ya wazabuni yaliyohakikiwa na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali (IAG) na kukidhi vigezo ikiwa ni sawa na asilimia 73.

 

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Ritha Kabati alietaka kufahamu Serikali imewalipa wazabuni wangapi wanaozidai Taasisi mbalimbali nchini na kiasi gani kimelipwa.

 

Mhe. Chande alisema kuwa Idadi ya Wazabuni waliolipwa ni 8,830 ambao walikuwa wakidai Taasisi mbalimbali za Serikali. Ulipaji huo ni hatua ya Serikali katika kuchochea uchumi na kukuza sekta binafsi.

 

Alisema kuwa Serikali inaendelea kuwalipa wazabuni kwa kadri fedha zitakavyopatikana na pia ulipaji ni lazima ufuate taratibu kwa kuwa suala la zabuni hutolewa kwa mkataba na ni suala la kisheria.

 

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), alipokuwa akijibu swali bungeni jijini Dodoma la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Ritha Kabati alietaka kufahamu Serikali imewalipa wazabuni wangapi wanaozidai taasisi mbalimbali nchini na kiasi gani kimelipwa.

 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Fedha)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...