Serikali imetenga shilingi Bilioni Tano katika mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambapo kati ya fedha hizo, kiasi cha shilingi milioni 224,750,000/= zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la huduma ya usafishaji damu.
Kauli hiyo imebainishwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel leo Jijini Dodoma wakati akijibu maswali bungeni kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu
Aidha Dkt. Mollel amesema kuwa kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa, matatizo yatokanayo na utoaji mimba ni moja ya sababu inayochangia vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 10%.
Hata hivyo amesema madhara yanayotokana na utoaji wa mimba usio salama ni pamoja na uambukizo mkali wa mfumo wa uzazi (Septic Abortion) ambao unaweza kupelekea mgonjwa kutolewa mfuko wa uzazi na wakati mwingine kupoteza maisha.
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...