Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya kilimo (TADB), Frank Nyabundege, Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya Biashara (TCB), Adam Mihayo wakisaini mikataba ya kushirikiana katika utoaji wa mikopo kwa wakulima, Wafugaji na Wavuvi nchini. Mikataba hiyo imesainiwa leo Februari Mosi, 2024 jijini Dar es Salaam wakisuhudiwa na maafisha mbalimbali wa benki ya TADB na TCB.
Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya kilimo (TADB), Frank Nyabundege, Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya Biashara (TCB), Adam Mihayo wakionesha mikataba ya kushirikiana katika utoaji wa mikopo kwa wakulima, Wafugaji na Wavuvi nchini. Mikataba hiyo imesainiwa leo Februari Mosi, 2024 jijini Dar es Salaam wakisuhudiwa na maafisha mbalimbali wa benki ya TADB na TCB.
Kutokea kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria TADB Dkt, Edson Rwechungura, 
na Mkurugenzi wa Sheria TCB Mystica Mapunda Ngongi wakisaini mikataba ya kushirikiana katika utoaji wa mikopo kwa wakulima, Wafugaji na Wavuvi nchini. Mikataba hiyo imesainiwa leo Februari Mosi, 2024 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi  Mwendeshaji wa benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Frank Nyabundege akizungumza leo februari Mosi, 2024 jijini Dar es salaam, Mara baada ya Kusaini mkataba wa ushirikiano kati ya benki ya TADB na TCB.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Adam Mihayo akizungumza na waandishi wa habari leo februari Mosi, 2024 jijini Dar es salaam, Mara baada ya Kusaini mkataba wa ushirikiano kati ya benki ya TADB na TCB. 

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
SEKTA ya kilimo inaendelea kukua na kuongeza ajira kwa vijana na wanawake benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) kupitia mfuko wake wa dhamana wa wakulima wadogo (SCGS) imetoa rai kwa mabenki nchini kujitokeza kushirikiana nao ili kuboresha mikopo kwa wakulima wadogo.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Frank Nyabundege ameyasema hayo leo februari Mosi, 2024 jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi ya kutia sahihi ya makubaliano ya kuongeza mkataba wa ushirikiano na benki ya biashara Tanzania(TCB) kwa ajili ya kutoa dhamana ya mikopo ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Amesema mkataba ulioingiwa kati ya pande hizo mbili ni wa awamu ya pili utaiwezesha benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kuchagiza upatikanaji wa mitaji kwa wakulima kupitia benki ya Benki ya Biashara Tanzania (TCB).

"Mikopo itakayotolewa na TCB kwa wakulima watatoa kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo, mifugo na uvuvi na sisi TADB tutatoa dhamana ya hadi asilimia 70 kwa mikopo yote hasa kwa vijana, wanawake na miradi inayosaidia kupunguza au kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi." Amesema Nyabundege.

Ameongeza kuwa mkataba huo utasaidia kuongeza wigo wa upatikanaji wa mikopo kwa wakulima wadogo na itakua njia rahisi ya kuwafikia wengi zaidi hasa waliopo pembezoni mwa miji, mikoa na Wilaya.

Amesema mkataba huo walioingia leo ni wa awamu ya pili ambapo awamu ya kwanza TCB kupitia kupitia dhamana ya TADB ilitoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 34.1 kwa wanufaika wa moja kwa moja 2,638 na wasio wa moja kwa moja zaidi ya 7,750 ambapo zaidi ya asilimia 95 walikua wakulima wadogo.

Ameongeza kuwa TADB imefanya maboresho na imeongeza wigo wa dhamana kutoka asilimia 50 ya awali mpaka asilimia 70 kwa miradi ya wanawake, vijana na miradi ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo pia itasaidia upatikanaji wa mikopo na kuchochea ongezeko la ajira kwa vijana.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Adam Mihayo amesema kuwa mkataba huo utaongeza wigo wa kutoa mikopo na kuwafikia wakulima wengi zaidi katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Amesema mikopo hiyo itawasaidia kuwapa mitaji itakayowawezesha kutoka kwenye kilimo cha kujikimu na kwenda kwenye kilimo cha biashara kwa riba nafuu ambapo pia itasasaidia kuinua uchumi wa nchi kwa ujumla.

"Tunaishukuru TADB kwa kutuongezea nguvu kwa ajili ya kuwafikia wakulima, wafugaji na wavuvi wengi zaidi na mikopo hii itapatikana katika matawi yote ya TCB nchi nzima na nia hasa ya kuongeza mikataba hii ni kuhakikisha tunawafikia wakulima wa pande zote za muungano kwa kuwaongezea mitaji kwa riba nafuu." Amesema Mihayo

Ushirikiano wa TCB na TADB umefanya jumla ya taasisi za kifedha zinazonufaika na mfuko wa dhamana wa wakulima wadogo (SCGS) kufikia 16 ambapo mpaka kufikia mwezi Disemba 2023, jumla ya mikopo ilikuwa Shilingi Bilioni 250.77 kwa wanufaika wa moja kwa moja zaidi ya 19,400 na ambao sio wa moja kwa moja zaidi ya 897,900 kutoa mikoa yote Tanzania bara na Visiwani.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Adam Mihayo akizungumza na waandishi wa habari leo februari Mosi, 2024 jijini Dar es salaam, Mara baada ya Kusaini mkataba wa ushirikiano kati ya benki ya TADB na TCB.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Frank Nyabundege akizungumza leo februari Mosi, 2024 jijini Dar es salaam, Mara baada ya Kusaini mkataba wa ushirikiano kati ya benki ya TADB na TCB.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...