Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Bi. Rose Joseph, akitoa Maelezo kuhusu ushiriki wa Chuo Kikuu cha Dodoma, kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene.

Na.Mwandishi Wetu-ARUSHA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene,ametembelea Banda la Chuo Kikuu cha Dodoma, wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Nne (4) cha Serikali Mtandao eGA, kilichoanza leo mkoani Arusha.

Mhe. Simbachawene, amepongeza Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kushirikj, pamoja na ubunifu mzuri wa Wanafunzi kutoka Ndaki ya Sayansi za Komputa na Elimu Angavu(CIVE).

Chuo Kikuu cha Dodoma ni miongoni mwa wadhamini wa Mkutano wa Nne wa Serikali Mtandao, unaokutanisha Wakuu wa Taasisi, Maafisa TEHAMA, Wakurugenzi wa Mipango, Utawala, na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini. Kikao hicho kimeanza leo Jumanne tarehe 06 Februari na kinategemewa kumalizika Ijumaa tarehe 08 Gebruari 2024.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, akisaini kitabu cha wageni alipowasili kwenye Banda la Chuo Kikuu cha Dodoma- Arusha. Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Bi. Rose Joseph, akitoa Maelezo kuhusu ushiriki wa Chuo Kikuu cha Dodoma, kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, akifurahia jambo na Watumishi wa UDOM hawako pichani. Pembeni ya Waziri ni mwakilishi wa Bodi ya e-GA, Dr. Jasmine Sekwa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, alipokea Maelezo ya Bunifu za wanafunzi wa Ndaki ya Sayansi za Komputa na Elimu Angavu, walioshiriki kwenye maonesho yanayoendelea wakati wa kikao cha Nne cha Serikali Mtandao e-GA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...