Na Khadija Khamis. Maelezo. 29/02/2024.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita amewataka Wasanii Wazanzibar hasa wa Muziki kuchangamkia fursa mbali mbali zinazojitokeza ili kukuza vipaji vyao na kujitangaza.

Ameyasema hayo huko katika Ukumbi wa Hotel ya Kendwa Rock Nugwi wakati wa hafla ya kutangazwa Majina ya Wasanii walifanikiwa kushindania Tuzo ya muziki ‘‘Zanzibar International Music Wards 2023-2024”, inayotarajiwa kufanyika tarehe 27, April, mwaka huu.

Amesema, Wizara inachukua jitihada kubwa za kuona sanaa ya Zanzibar inapiga hatua na Wasanii wanaweza kufanya vizuri katika kazi zao.

Aidha amesema lengo la kuanzishwa tunzo hizo ni kuwapa moyo na hamasa Wasanii wa Zanzibar ili kufanyakazi ya Sanaa kwa malengo na kuwa chachu ya mabadiliko.

“Natamani kuona wasanii wa Zanzibar wanashinda vipengele ambavyo vimetajwa lakini pia kuona wanachangaamkia fursa hii kwani hii ni moja ya kuwatia moyo wa mafanikio,” alisema Waziri Tabia.

Waziri Tabia aliwapongeza wasanii wote wa Zanzibar na Tanzania bara kwa ujumla walioingia kuwania tunzo hizo na kutaka mchakato wa upigaji kura uwe wa wazi ili kuepusha malalamiko ambayo yanaweza kujitokeza.

Pia Waziri Tabia amesikitishwa na wasanii wa utamaduni kwa kushindwa kutojitokeza jambo ambalo limepelekea kufutwa baadhi ya vipengele.

Aidha amevitaja vipengele vilivyofutwa kuwa ni pamoja na Kikundi bora cha utamaduni, Msanii bora wa utamaduni, Mnenguaji bora wa kike wa muziki wa dansi wa mwaka na Mnenguaji bora wa Kiume muziki wa dansi.

Hata hivyo amelitaka Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar kukutana na kuvihamasisha vikundi vya utamaduni vilivyopo nchini ili kuweza kukusanya taarifa za kazi zao na kuziwasilisha kwa ajili ya tunzo zijazo.

Vile vile ameitaka kamati hiyo kuhakikisha inavitumia vyombo vya habari vya ndani na nje ya Zanzibar katika kutangaza namna bora ya upigaji wa kura katika tuzo hizo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Tunzo hizo ambae pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar Ramadhani Bukini amesema jumla ya vipenge 24 vya Wasanii vinatarajiwa kugombania tuzo hizo.

Alisema kamati ilipitisha vipengele 24 kwa kufuata mchakato sahihi ikiwemo kushirikiana na Baraza la Sanaa hapa Zanzibar pamoja na lile la Tanzania bara “Basata.” na wasanii wenyewe.

Alisema wasanii wengi wa Zanzibar walijitokeza kupeleka kazi zao kwa kutumia mfumo maalum ambao ndio uliokuwa ukipokea kazi hizo.

Amefahamisha kuwa mchakato wa kuwapigia kura wasanii hao utaanza leo Saa sita kamili usiku kupitia code ya kila Msanii ili kuona mtu anaweza kupiga kura moja.

Miongoni mwa vipengele hivyo ni pamoja na Mtunzi bora wa Mwaka, Dj bora wa Mwaka, Kundi bora la unenguaji, Mpiga Ala ya muziki bora wa mwaka, Msanii bora wa kike na wakiume wa Afrika Mashariki, Mtayarishaji wa Muziki wa Mwaka, Muimbaji bora wa kike na wakiume wa Tarab Asilia, Muimb aji bora wa kike wa taarab wa mwaka, Muimbaji bora wa kike Zenji flevana Muimbaji bora wa kiume wa taarab wa mwaka.

Vipengele vingine ni Muimbaji bora wa kiume wa zenji fleva wa mwaka, Wimbledon bora wa kushirikiana wa mwaka, Wimbledon bora wa Hip hop wa mwaka, Wimbledon bora wa Afrika Mashariki wa mwaka, Wimbledon bora wa Taarab wa mwaka, Video bora wa muziki wa zenji fleva, video bora ya muziki wa modern taarab.Mwanamuziki bora Chipukizi wa Mwaka, Muongozani bora wa video ya muziki wa mwaka, Wimbo bora wa taarab Asilia na Wimbo bora wa Zenji fleva wa mwaka.

Alieleza kuwa tunzo hizo zinasimamiwa na Wizara ya Habari,Vijana , Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Mamlaka ya mapato Zanzibar (ZRA), Benki ya Watu wa Zanzibar(PBZ) na Hotel Kendra Rock.

Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia  Maulid Mwita akizungumza katika hafla ya kuwatangaza  wasanii waliofanikiwa kushindania tuzo mbalimbali za muziki (Zanzibar Internal Music Award) huko Kendwa Rocks Mkoa wa Kusini Unguja.

PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...