Katibu Tawala Wilaya ya Nachingwea Mbarouk Balozi amefunga mafunzo ya uongozi, usimamizi na uendeshaji wa shule za msingi yaliyoendeshwa kwa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi za Mikoa wa Simiyu, Kigoma, Tanga, Kilimanjaro, Mbeya na Mtwara chini ya mradi wa BOOST na kusimamiwa na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM)

Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri Elekezi -ADEM Dkt. Alphonce Amuli ameeleza kuwa hadi sasa ADEM imeshatoa mafunzo kwa walimu wakuu 4,522 katika awamu ya kwanza ya mafunzo hayo, na katika awamu hii mafunzo hayo yametolewa kwa Walimu Wakuu 4,620 katika Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Simiyu, Mbeya, Kigoma na Mtwara
Baadhi ya walimu wakuu walioshiriki mafunzo hayoNa Fredy Mgunda,Lindi

Katibu Tawala Wilaya ya Nachingwea Mbarouk Balozi amefunga mafunzo ya uongozi, usimamizi na uendeshaji wa shule za msingi yaliyoendeshwa kwa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi za Mikoa wa Simiyu, Kigoma, Tanga, Kilimanjaro, Mbeya na Mtwara chini ya mradi wa BOOST na kusimamiwa na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM).


Akizungumza katika ufungaji wa mafunzo hayo, Balozi amewataka walimu hao kwenda kuboresha utendaji kazi katika vituo vyao vya kazi kwa kihakikisha wanasimamia kikamilifu shughuli za ufundishaji na ujifunzaji shuleni kwa ubora.


"ADEM imemaliza kazi yake ya kuendesha mafunzo haya kwa walimu wakuu katika Mikoa sita nchini, ni wajibu wa Walimu Wakuu mliopatiwa mafunzo haya kwenda kuyatumia katika utendaji wenu wa kila siku ili kufikia adhma ya Serikali ya kuboresha elimumsingi nchini" Amesema. Balozi

Balozi aliwataka Walimu Wakuu kuongoza shule kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma na kusimamia miradi ya elimu wanayotakiwa kusimamia kwa ufanisi kwani kupitia mafunzo hayo wamejengewa uwezo kuhusu usimamizi wa rasilimali za shule hususani fedha na miradi ya ujenzi inayotekelezwa shuleni.

Balozi alimalizia kwa kuupongeza uongozi wa ADEM kwa kuendesha mafunzo hayo kwa umahiri mkubwa na kuwataka kuendelea kuendesha mafunzo hayo kwa umahiri huo huo katika Mikoa iliyobaki.


Nae Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri Elekezi -ADEM Dkt. Alphonce Amuli ameeleza kuwa hadi sasa ADEM imeshatoa mafunzo kwa walimu wakuu 4,522 katika awamu ya kwanza ya mafunzo hayo, na katika awamu hii mafunzo hayo yametolewa kwa Walimu Wakuu 4,620 katika Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Simiyu, Mbeya, Kigoma na Mtwara kuanzia februari 15 hadi machi 13, 2024.


Dkt. Amuli aliwataka walimu kutumia mafunzo hayo katika kuboresha utendaji na usimamizi wa shule ili kuleta tija na thamani ya fedha iliyotumika kuyaendesha ionekane.


alisema kuwa Lengo la mafunzo ni kumjengea uwezo Mwalimu Mkuu kutekeleza majukumu yake ya kusimamia shule hususani katika kuhakikisha shughuli za shule zinafanyika kwa ubora na ufanisi unaotakiwa. Mwalimu Mkuu ni mtendaji muhimu katika ngazi ya shule.

Dkt. Amuli alisema kuwa baada ya mafunzo hayo, washiriki watafuatiliwa na kupimwa katika maeneo yote waliyowezeshwa,Miongoni mwa viashiria vya utekelezaji wa mafunzo kwa Mwalimu Mkuu ni pamoja na uwepo wa taarifa zifuatazo,Mpango wa Jumla wa Maendeleo ya Shule,Mpango wa kushughulikia malalamiko kwa Watumishi, wanafunzi na jamii,Mpango wa Motisha kwa wafanyakazi na wanafunzi,Miundombinu bora ya shule,Matokeo chanya ya ujifunzaji na ufundishaji shuleni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...