Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Mradi wa Airtel Smart Wasomi umekuja wakati muafaka, wakati Serikali ikitekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la 2023 ambapo matumizi ya Tehama katika mifumo ya Elimu yamepewa kipaumbele.

Prof. Nombo mwishoni mwa wiki jijini Dodoma katika halfa ya utiaji saini hati ya makubaliano ya ushirikiano wa Mradi huo kati ya Airtel, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), akisema Mradi huo utaleta faida kubwa katika sekta ya Elimu kwa kuboresha upatikanaji wa maudhui ya elimu kwa njia ya mtandao na dijitali.

Prof. Nombo ameipongeza Kampuni ya Airtel pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kuja na Mradi huo unaoakisi malengo ya serikali katika kutoa huduma jumuishi ya Elimu kidijitali na kwamba utaongeza ari ya ujifunzaji na kuleta matokeo chanya ya ufaulu kwa Wanafunzi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Celestine Kakele ameeleza kuwa moja ya wajibu wa msingi wa serikali ni kutoa huduma za kijamii ikiwemo elimu katika kutekeleza jukumu hilo inahakikisha usalama na utolewaji wa huduma bora na jumuishi katika Nyanja ya Mawasilino.

‘’Naipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambayo ina jukumu la kusimamia Sera na kuratibu maendeleo ya Sayansi na Teknolojia pomoja na Ofisi ya TAMISEMI ambayo inasimamia masuala ya miundombinu ya elimu kwa kushirikiana kampuni ya Airtel kutekeleza mradi huu wa kuziunganisha shule zetu na teknolojia ya mawasiliano’’ alisema Kakele.

Akimwakilishi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Emmanuel Shindika amesema Mradi huo umeleta historia katika kuijenga Tanzania ya kidijitali kupitia elimu na kwamba itawasaidia Walimu kupata maudhui kwa urahisi na hivyo kuboresha ufundishaji.

‘’Malengo ya Serikali kupitia TAMISEMI ni kuhakikisha shule zetu zinakuwa na miundombinu stahiki ya utoaji elibu bora ili kufikia malengo hayo moja ya miundombinu muhimu katika karne hii ya 21 ni TEHAMA’ alisema Dkt. Shindika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Dinesh Balsingh, amesema Mradi huo utawezesha ufundishaji na upatikanaji wa maudhui kidigitali katika Shule za Serikali takriban 3,000 ndani ya miaka miatano.

Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa Kampuni hiyo inaamini elimu ni haki ya msingi kwa kila mtoto, na hivyo inawajibika kushirikiana na Serikali kuboresha ubora wa ujifunzaji katika Shule za Sekondari Nchini ili kufikia lengo namba Nne la agenda ya maendeleo endelevu.

Nae Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Bi. Elke Wisch ameipongeza Serikali Tanzania kufikia hatua hiyo muhimu katika kuboresha matokeo ya kujifunza kwa kutumia huduma za kidijitali katika mfumo wa elimu.

Aidha amesema hatua ya makubaliano hayo unaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye Maktaba ya mtandaoni, na kwamba Shirika hilo litaendelea kusaidia uimarishaji wa Elimu ya kidigitali kwa kubuni mifumo rafiki na ya gharama nafuu.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Dinesh Balsingh (wa pili kushoto) wakibadilishana hati za makubaliano ya ushirikiano wa mradi wa ‘Airtel Smart Wasomi’ mara baada ya kusainiwa kwa hati hizo. Programu hiyo ya Airtel ‘Smart Wasomi’ inatarajiwa kuwezesha shule zaidi ya 3000 nchini kuunganishwa na mifumo ya kufundishia kidijitali. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dodoma katika Ofisi za Wizara ya Elimu. Wengine ni Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini, Bi. Elke Wisch (kulia), Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk. Emmanuel Shindika (wa pili kulia) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Selestine Kakele. (Picha na Airtel)
 Mwakilishi Mkazi wa UNICEF nchini, Bi. Elke Wisch (kulia) akishuhudia Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo (katikati), Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk. Emmanuel Shindika (wa tatu kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Dinesh Balsingh wakisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano wa mradi wa ‘Airtel Smart Wasomi’. Programu hiyo ya Airtel ‘Smart Wasomi’ inatarajiwa kuwezesha shule zaidi ya 3000 nchini kuunganishwa na mifumo ya kufundishia kidijitali. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dodoma katika Ofisi za Wizara ya Elimu. (Picha na Airtel).
 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...