Na. Vero Ignatus, Arusha

Wakulima wametakiwa Wakulima watakiwa kununua mbegu bora kwa mawakala waliosajiliwa na kuacha tabia ya kununua mbegu minadani kibolela.

Hayo yamesemwa na wataalamu wa sayansi ya mimea wa kampuni ya Balton Tanzania inayoingiza na kusambaza mbegu katika mafunzo kwa zaidi ya wakulima 300 kutoka mikoa Geita, Iringa, Mbeya,Morogoro,Mwanza,Shinyanga,na Tabora kuwa ni muhimu kwao kununua mbegu zilizothibitishwa.

Akizungumza na wakulima Afisa Mfawidhi wa Taasisi ya Kuthibiti Ubora wambegu Tanzania, Kanda ya Kaskazini, Dk Munguatosha Ngumuo alisema wakulima wanapaswa kuacha kilimo cha mazoea badala yake wajifunze kulima kisasa kwa kutumia mbegu bora.

Mkurugenzi Mtendaji wa Balton Tanzania Chris Keeping aliwataka wakulima hao kuwa kufahamu aina ya mbegu inayofaa kulima katika ukanda waliopo pamoja na kujifunza namna ya kudhibiti wadudu kuwasaidia kupata mazao mengi Kwa wakulima hao.

Amesema kuwa kufanya kilimo chenye tija hususani kipindi hiki cha athari ya mabadiliko ya tabia ya nchi kutapelekea kuwa na chakula cha kutosha nchini na ziada kuuzwa nchinza nje.

Mtaalamu wa sayansi ya Mimea wa BaltonTanzania Halima Amir alisema wakulima wanatakiwa kutumia mbegu sahihi na kulima kwa kuzingatia utaalam.

Wakulima Paulo Nko wa Ngaramtoni wikaya ya Arumeru na Hapiness Kaweji kutoka Tarakia mkoani Kilimanjaro walipongeza elimu iliyotolewa na Balton katika kuboresha kilimo chao.

Mafunzo hayo ya siku tatu yanatolewa na kampuni ya kuuza mbegu ya Balton Tanzania ambayo pia yameshirikisha mawakala wa mbegu nchini na wataalam wa kilimo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Balton Tanzania Chris Keeping a kuzungumza na wakulima.aina bora ya  mbegu inayofaa kwa kilimo ukanda waliopo
Afisa mfawidhi kanda ya kaskazini wa taasisi ya uthibiti wa ubora wa mbegu nchini Dkt. Munguatosha Ngomuo nchini .
Wakulima wakiwa wanafuatilia mafunzo kwa makini namna ya mbegu Bora katika ukanda wao
Mtaalamu wa sayansi ya Mimea wa BaltonTanzania Halima Amir  akuzungumza na wakulima

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...