Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa, akiwa na wanafunzi wa kike waliofanya vizuri katika somo la hisabati muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi za laptop kutoka Barrick.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk. Franklin Rwezimula (kushoto) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa kwa niaba ya kampuni.
Mmoja wa wasichana waliofanya vizuri katika somo la hisabati, kutoka sekondari akipongezwa baada ya kupokea zawadi la Laptop kutoka Barrick
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari mkoani Morogoro walishiriki katika maadhimisho hayo
Wanafunzi wakishiriki kujibu maswali ya chemshabongo katika hafla hiyo.
---
Kampuni ya dhahabu ya Barrick nchini, imedhamini madhimisho ya Siku ya Hisabati Duniani ambapo kwa hapa nchini yalifanyika mkoani Morogoro kwa kuandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania ambacho kinashirikiana na Serikali kuongeza ufaulu wa masomo ya hisabati katika shule za msingi na Sekondari nchini.

Kwenye kilele cha maadhimisho hayo , Barrick ilieleza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha elimu nchini ikiwemo kufanikisha ufaulu wa masomo ya sayansi na TEHEMA mashuleni ili taifa lisibaki nyuma katika ulimwengu wa sayansi ya teknolojia

Pia imedhamiria kutoa hamasa na motisha kwa watoto wa kike watakaofanya vizuri katika masomo ya sayansi na kutoa wito kwa wasichana kujiamini na kuondoa dhana ya kwamba masomo ya sayansi ni kwa ajili ya wavulana.

Katika hafla hiyo wanafunzi wa kike watatu waliofanya vizuri katika somo la hisabati lililoandaliwa na Chama cha Hisabati nchini mwaka jana walizawadiwa na laptop za kisasa kila mmoja na kampuni ya Barrick .Wanafunzi hao wanatokea katika sekondari za Lumumba-Zanzibar,Canosa na Marian.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk.Franklin Rwezimula, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, alisema Serikali inaendeea kufanya mikakati mbalimbali kuhakikisha ufaulu wa somo la hesabu na masomo mengine ya sayansi unaongezeka na aliwapongeza wadau mbalimbali wanaounga mkono jitihada za Serikali katika kufanikisha suala hili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...