Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeandaa hafla ya futari mahususi kwa wateja wake wa Kiislamu Zanzibar. Hatua hiyo ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuandaa hafla za namna hiyo maeneo mbalimbali hapa nchini ikilenga kuonyesha mshikamano na umoja katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hafla hiyo imefanyika jana kwenye hotel ya Madnat Al  Bahr, Zanzibar ikiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi -Zanzibar , Zubeir Ali Maulid.  Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, La Riba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Raymond Urassa alimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Theobald Sabi  kwenye hafla.

Katika hotuba yake, kwenye hafla hiyo hiyo iliyohudhuriwa na wageni mbalimbali waalikwa wakiwemo viongozi waandamizi serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Wajumbe wa baraza la wawakilishi, wabunge na wateja wa benki hiyo, Spika Zubeir alipongeza benki ya NBC kwa ushirikiano wake na wadau wake huku akisisitiza umuhimu wa mahusiano yanayogusa na kuheshimu misingi ya imani za dini kwa wateja wa benki.

Kwa upande wake Urassa alisisitiza juu ya umuhimu wa uhusiano mzuri kati ya benki na wadau wake muhimu ikiwemo Serikali na wateja. Alitumia fursa hiyo kuzungumzia huduma maalum inayotolewa na Benki ya NBC kwa wateja wa Kiislamu inayojulikana kama La Riba, ambayo inazingatia mafundisho ya Kiislamu kuhusu riba.

Hafla hiyo pia ilihusisha utoaji wa zawadi kwa wageni waalikwa. Kwa wateja wa Kiislamu wa benki ya NBC visiwani Zanzibar, hafla hiyo ilikuwa fursa nzuri ya kufurahi pamoja na kujenga uhusiano mzuri miongoni mwao na benki hiyo.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid  (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla  ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid akiwaongoza wageni wengine waalikwa pamoja na wafanyakazi wa benki ya NBC  kupata chakula wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, La Riba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Raymond Urassa (Katikati) akimkabidhi Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid  (kushoto) zawadi maalum wakati wa hafla futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, La Riba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Raymond Urassa (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla  ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Zanzibar Bw  Ramadhani Lesso (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla  ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Meneja wa Benki ya NBC  Kanda ya Pwani Bi Zubeider Haroun (katikati) sambamba na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa hafla  ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid (kushoto) akiwaongoza wageni wengine waalikwa pamoja na wafanyakazi wa benki ya NBC  wakati wa ibada ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani Zanzibar. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zubeir Ali Maulid  (wa saba kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC  Zanzibar wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani humo. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Mke wa Spika Mama Warda Zubeir  (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC  Zanzibar wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani humo. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Ramadan Kareem! Wafanyakazi wa benki ya NBC Zanzibar wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake visiwani humo. Hafla hiyo ilifanyika jana visiwani humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...