Na Mwandishi wetu

Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) limesaini makubaliano na kampuni ya Bravo Group ya kutumika kwa Reli ya TAZARA kusafirisha mizigo kati ya Tanzania, Zambia, Kongo, Zimbabwe na Afrika Kusini.

Tazara imeingia makubaliano hayo kama sehemu ya utekelezaji wa azimio la mageuzi ya kiuchumi kwenye sekta ya usafirishaji kupitia reli ikiwa Tanzania ni miongoni mwa Mataifa ulimwenguni yenye uhitaji mkubwa wa usafirishaji wa bidhaa zinazoingia nchini kupitia Bandari ambapo kuingia kwa bidhaa hizo kunatoa mianya ya kuhitajika usafirishaji kwenda nchi jirani.

Mkurugenzi mtendaji wa TAZARA, Eng. Bruno Tadeo Ching'andu amesema kuwa makubaliano haya yataboresha zaidi biashara ya TAZARA, kwake anaona kutakua na biashara kubwa zaidi ukilinganisha na biashara waliyonayo kwa sasa.

Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Bravo Group, Angelina Ngalula amesema anashukuru juhudi za Mheshimiwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Tanzania inakua kitovu cha usafirshaji mizigo kwa ukanda wa SADC.

Ngalula amesema ‘Mipango hii ingeanza muda kidogo toka 2021 bahati mbaya miundombinu ya TAZARA haikua rahisi kwa kampuni nyingine kuingiza treni ili kupishana, Kwa sasa tutaanza na treni 2 ambazo zitakua zinapishana, treni moja itakua na behewa 20 na kila behewa litabeba tani 50 ambapo jumla tani 1,000 sawa na malori 40 zitabebwa kwa pamoja, na kwa ujumla treni hizi mbili ni sawa na lori kubwa 80, Kadri TAZARA watakavyoongeza njia sisi tutaingiza treni nyingi zaidi’ - Ngalula.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...