Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba, nchini Tanzania, Mhe. Yordenis Despaigne Vera. Katika Mazungumzo hayo Dr. Nchimbi na Mhe. Balozi Vera wamejadiliana juu ya masuala mbalimbali yanayohusu namna ya kuimarisha zaidi uhusiano kati ya Tanzania na Cuba na Chama Cha Mapinduzi na Chama Cha Kikomunisti cha Cuba (CPC).

Wakati wa Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam, leo Jumamosi Machi 5, 2024, Mhe. Balozi Vera ameishukuru Tanzania na CCM kwa jinsi ambavyo daima wamesimama na nchi hiyo katika nyakati zote.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Nchimbi amemhakikishia Mhe. Balozi Vera kuwa CCM, chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, kitafanya kila linalowezekana kuhakikisha urafiki na uhusiano kati ya Tanzania na Cuba kwa upande mmoja na CPC na CCM kwa upande mwingine unaenziwa na kuimarishwa zaidi kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili.

Kupitia majadiliano hayo, pamoja na masuala mengine, viongozi hao wa pande zote mbili, wamejadiliana na kuainisha maeneo yatakayofanyiwa kazi kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha ushirikiano kati ya Wananchi wa Tanzania na Wananchi wa Cuba, Serikali za nchi zote mbili na vyama vinavyoongoza nchi hizo, huku wakisisitiza umuhimu wa kuendeleza mipango ya kubadilishana utaalam katika maeneo mbalimbali na kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya kiuchumi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Mhe. Yordenis Despaigne Vera, walipokutana kwa ajili ya mazungumzo leo Jumanne, Machi 5, 2024, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...