Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko, Leo 27 Machi, 2024, ameshuhudia Utiaji saini mikataba mitatu ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

Mkataba wa Kwanza unahusisha ukodishaji wa eneo la kujenga Miundombinu ya kuhifadhi mafuta (Land Lease Agreement for Marine storage and Terminal Area) Kati ya TPDC na EACOP.

Mradi wa pili ni wa kutumia eneo la Maji (Marine user Rights) kati ya EACOP na Mamlaka ya Bandari Tanga na mkataba wa tatu ni wa kufanya shughuli za Bandari (Marine Facility Agreement) Kati ya TPA na EACOP.

Utiaji saini mkataba huo pia umeshuhudiwa na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda Mhe Dkt. Ruth Nankabirwa.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...