Benki ya Exim imeandaa futari ya pamoja kwa wateja wake katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 15 mwezi Machi 2024.

Mgeni Rasmi katika tukio hili alikuwa Sheikh Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, akiwakilisha waumini wa dini ya Kiislam ambao wapo kwenye mfungo katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, aliipongeza Benki ya Exim kwa juhudi zake katika kukuza maendeleo ya kijamii na kueleza shukrani zake kwa mchango wa benki hiyo kwa jamii. Alisema, “Benki ya Exim inaonyesha dhamira ya kweli katika kutumikia wateja wake na jamii kwa ujumla, lengo kuu la Ramadhani ni kuleta watu pamoja, na usiku huu, benki ya Exim imehakikisha kuendeleza lengo hilo kwa vitendo”.

Bwana Jaffari Matundu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, aliwakaribisha wadau wote katika Iftar hiyo huku akitambua mahusiano mazuri ya tija yaliopo baina ya Benki ya Exim na wateja wake na umuhimu wa kuyaendeleza kwa ajli ya ustawi na maendeleo ya jamii.

“Wateja wetu ni zaidi ya wateja tu, ni sehemu muhimu ya familia yetu. Tunaona kila mmoja wenu kama mshirika na mwenzetu katika safari yetu ya mafanikio”, alisisitiza Jaffari Matundu.

Pia, Mkurugenzi huyo alizungumzia hatua na maboresho mbalimbali ambayo yamefanywa na benki ya Exim ili kuendana na mabadiliko katika sekta mbalimbali ikiwemo maendeleo ya teknolojia ya kidijitali na kusogeza huduma kwa wateja.

Jaffari alifafanua kuwa, “tumefanya maboresho makubwa katika mfumo wetu wa Benki ili kuendelea kuhudumia wateja wetu vizuri zaidi kwa kutoa huduma zinazoendana na mabadiliko ya kidigitali”.

“Vile vile tumeendelea kuongeza idadi ya Mawakala wetu (maarufu kama Exim Wakala) ili kuleta huduma zetu karibu na wateja wetu popote walipo”, alimalizia Afisa Mtendaji Mkuu huyo.

Exim Bank pia imeboresha huduma za kidijitali kwa wateja wake ambapo wanaweza kupata huduma za kibenki popote pale walipo ndani na nje ya Tanzania. Hii ni kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa wateja wao na maendeleo ya teknolojia yanayoendelea kutokea duniani.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Jaffari Matundu, akizungumza na wadau (hawapo pichani) katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya benki na wadau wake wakiwemo wateja na jamii katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani katika tukio lililofanyika tarehe 15 Machi 2024 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, akitoa pongezi kwa Benki ya Exim kwa kuandaa Iftar akielezea namna ambavyo imewaleta pamoja waumini wa dini ya kiislam kama ishara ya upendo, umoja na heshima kwa wadau wote katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 15 Machi 2024 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu (wa tatu kutoka kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar (watatu kutoka kulia) wakiwa na baadhi ya viongozi wa Exim Bank wakipata futari iliyoandaliwa na benki hiyo tarehe 15 Machi 2024 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali na wawakilishi wa Benki ya Exim wakifurahia Iftar iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwaleta pamoja katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani kuashiria furaha, umoja, na upendo katika tukio lililofanyika tarehe 15 Machi 2024 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam

Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam Sheikh Walid Alhad Omar (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Exim Bank, Jaffari Matundu (watatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa benki hiyo wakati wa hafla ya Iftar iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwakutanisha wateja wake pamoja katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani iliyofanyika tarehe 15 meezi Machi 2024 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...