Na Mwandishi Wetu Bungeni Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Florent Laurent Kyombo akikaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo hii leo Machi 20, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge Jijini Dodoma mara baada ya wajumbe kujadili na kuridhia Bajeti katika kikao kilichohusisha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.


Alisema baada ya majadiliano mazuri na maelezo ya ziada kutolewa kuhusiana na Bajeti iliyotengwa, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria imeridhia. 


“Tunawatakia matumizi mema ya fedha hizi pale zitakapokubaliwa kupitishwa katika vikao vya Bunge la Bajeti na tunahitaji kuona Bajeti ya fedha hizi inaakisi matarajio ya msingi ya nchi yetu,” alibainisha.

Kwa Upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderiananga akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ameishukuru kamati kwa ushauri na kupitia Bajeti hiyo kifungu kwa kifungu na kutoa maelekezo ambayo yatasaidia Bajeti hiyo kukaa vizuri wakati kusomwa Bungeni kwenye vikao vya Bunge la Bajeti.
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama akizungumza wakati wa uwasilishaji wa taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mwaka wa fedha 2024/25.
 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)  Ummy Nderiananga akizungumza jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mwaka wa fedha 2024/25.
 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria  Florent Laurent Kyombo (akikaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo) ameongoza kikao cha kamati hiyo katika Ukumbi wa Bunge kilichopokea Taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mwaka wa fedha 2024/25
 

Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2024/25.
 

Kaimu Kamishina Jenerali Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Shaaban Mbaraza akiongea jambo katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mamlaka kwa mwaka wa fedha 2024/25.

 

Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria wakifutilia kwa makini taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa mwaka wa fedha 2024/25

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...