Na mwandishi wetu Tanga

Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo leo tarehe 16 Machi, 2024 jijini Tanga wamehitimisha ziara yao ya siku mbili kwa Kupokea na Kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Ujenzi wa Mnada wa Mifugo wa Mpakani wa Horohoro katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga.

Mradi huo ulijumuisha ujenzi wa mazizi 4, kishushio na kipakilio, kiringe, banda la mbuzi lenye uwezo wa kuchukua mbuzi 500, birika la kunyweshea mifugo, kujenga jengo la vyoo vya matundu 6 na kuunganisha mnada na huduma za umeme na maji.

Aidha, Mwenyekiti pamoja na wajumbe waliipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na watendaji wa Halmashauri hiyo kwa ujenzi wa mnada mzuri ambao utachochea ari ya maendeleo ya Halmashauri. Mwenyekiti aliendelea kwa kuwasisitiza kukamilisha ujenzi wa mnada huo ikiwa ni pamoja na kuleta maji mnadani hapo.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...