Na Mwandishi wetu

Serikali kupitia Halmashauri ya wilaya ya Songea Vijijini yaahidi kushughulikia na kuupatia ufumbuzi mgogoro wa ardhi katika kitongoji cha Msiri na Hifadhi ya Maliasili kilichopo katika kijiji cha Nakahengwa.

Kauli hiyo ameitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama (Mb) Peramiho, katika kijiji cha Nakahengwa Wakati akimnadi Mgombea Udiwani Optatus Ndalu, ambapo uchaguzi mdogo unatarajiwa kufanyika tarehe 20/03/2024 baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo ya Mbinga Mhaule kufariki.

Aliongeza kusema tumejipanga kuhakikisha migogoro yote ya ardhi katika Kijiji cha Nakahengwa inamalizika na watu wanaishi kwa Amani.

"Tunahitaji kuona kila mgeni anayeingia katika Kijiji cha Nakahengwa, hafikirii kuondoka kwa sababu wenyeji wa hapa ni wakarimu na Wenye upendo," alisema

Katika hatua nyingine Waziri Mhagama amewakumbusha wananchi umuhimu wa kuchagua Mgombea wa udiwani atakayeendelea kuchochea miradi ya maendeleo na kusimamia vyema ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Alikumbusha kuhusu uchaguzi Mkuu uliopita wa mwaka 2020, tuliomba mchague Mafiga Matatu ya Chama Cha Mapinduzi ili tujipange sawa sawa katika kushughulikia matatizo ya wananchi.

"Serikali kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi imeshaanza kushughulikia bei ya mbolea kwa kuhakikisha inaendelea kushuka ili kusaidia wananchi, " alibainisha

Muunganiko wa Mafiga haya matatu unaongozwa na Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umesaidia katika kupandisha bei ya mahindi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Songea Vijijini Thomas Masolwa amesema ujenzi wa Miundo Mbinu bora ya barabara, Miundo Mbinu ya Afya, Miundo Mbinu ya elimu na Nishati ya umeme inasimamiwa na ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Sasa tunatembea na ajenda ya kuziba pengo katika Kata ya Mbinga Mhalule kwa kutafuta Mtu atakayendelea kusimamia na kuchochea miradi ya Maendeleo kwa Wananchi.

"Kumpigia Kura Mgombea wa Chama cha Mapinduzi ni kupigia Kura maendeleo yanayoendelea kutekelezwa na Serikali," alibainisha

Naye Mgombe wa Chama Cha Mapinduzi Optatus Ndau ameahidi kuendelea kusimamia miradi yote inayotekelezwa katika kata ya Mbinga Mhalule.

Sambamba na hilo Ndau ameahidi kuendelea kusimamia migogoro yote ya ardhi ya mashamba na mipaka katika kata ya Mbinga Mhalule

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akimuombea Kura na kumnadi Mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM Optatus Ndau katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika Kijiji cha Nakahegwa kata ya Mbinga Mhalule.

 

Viongozi wa CCM wa wilaya ya Songea Vijijini na Wananchi wa kijiji cha Nakahegwa wakiongozwa na vijana wa usafirishaji abiria kwa pikipiki (boda boda) wakimlaki Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho kabla ya Mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji cha Nakahengwa.
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akiwa amembeba mtoto Wakati akizungumza na wakinamama wa Kijiji cha Nakahengwa kabla ya Mkutano wa Kampeni uliofanyika katika Kijiji hicho.

Wananchi wa Kijiji cha Nakahegwa wakiwa wamembeba kwa furaha Mgombe wa udiwani katika kata ya Mbinga Mhalule kwa tiketi ya CCM  Optatus Ndau Wakati wa Mkutano wa Kampeni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...