NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), imeridhishwa na uwekezaji wa jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex, lililoko barabara ya Sam Nujoma, jijini Dar es Salaam.

Jengo hilo la kisasa lenye ghorofa 35 linamilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na kwa sasa tayari limekamilika kwa asilimia 100 na limeanza kutumika.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa ziara ya PIC ya kutembeela mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 232, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge Mhe. Deus Sangu amesema, Kamati imekagua mradi na kujiridhisha kuwa ni mzuri na umetekelezwa kwa viwango vyote vinavyohitajika.

“Sisi kama kamati tumeendelea kuishauri PSSSF kuhakikisha jengo hili ambalo limewekeza fedha nyingi za Mfuko linasimamiwa na tija iliyokusudiwa inapatikana, tumekagua na tumeridhika na uwekezaji huu na tunaiponegza PSSSF.” Amesema.

Amesema Kamati yake imeelekeza katika kipindi cha matarajio ya chumo la uwekezaji (Return of investment) inaleta tija na kupata chumo ndani ya muda iliyojiwekea kisha kuanza kupata faida.

“Na hii itakuwa ni faida kwa Mfuko na kuufanya uweze kuendelea kuwahudumia wananchama bila kutetereka.” Alisema.

Mwenyekiti huyo amempngeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa namna anavyosukuma mabadiliko ya kiuchumi nchini na uwekezaji huo umeakisi R mbili kati ya zile nne za Mhe. Rais ambazo ni Reforms na Rebuild.

Naye Mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Pius Chaya, licha ya kupongeza uwekezaji huo lakini pia ameishauri serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina kuangalia uwezekano wa taasisi za umma ambazo ziko Dar Es Salaam kutumia jengo hilo.

“Hatuui taasisi binafasi lakini ipo haja ya kujaza nafasi zilizobaki.” Amefafanua Dkt. Chaya.

Akitoa wasifu wa jengo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru amesema jengo la PSSSF Commercial Complex ni jengo refu zaidi na ni moja ya alama za jiji la Dar Es Salaami, ni jengo refu sana katika nchi za Afriak Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Amesema jengo hilo lina minara mmitatu (towers) moja ni Commercial Complex ambalo ni refu zaidi lenye ghorofa 35 Executive tower lenye ghorofa 14 na eneo la maegesho lenye ghorofa 6.

“Hapa ndio panaitwa PSSSF Commercial Complex, kuna Executive tower ambako ni maalum kwa shughuli za maofisi, commercial complex linahusisha mabenki, ofisi mchanganyiko na kumbi za mikutano na shughuli nyingine za kijamii, lakini pia kuna ene la maegesho ya magari.” Amefafanua.

Amesema jengo hilo limeendelea kuwavutia wapangaji wengi zaidi kadiri muda unavyokwenda na matarajio ya Mfuko, kufikia desemba mwaka huu 2024, kiwango cha upangishaji kinatarajiwa kupanda na kufikia asilimia 70.

Amesema, miongoni mwa wapangaji mashuhuri kwenye jengo hilo ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa (UNDP) na taasisi zake, kampuni kubwa ya mitandao ya simu Tigo, taasisi za umma, mabenki na wafanyabiashara binafsi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), Mhe. Deus Sangu, akizungumza mara baada ya Kamati yake kukagua mradi wa jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex, lililoko barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam, Machi 21, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru, akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar Es Salaam, mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), wakati wa ziara ya wajumbe wa kamati ya PIC kukagua jengo, Machi 21, 2024.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji PSSSF, Bw. Rashid Mtima (Aliyesimama), akizungumza mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), Mhe. Deus Sangu (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru, wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), kukagua jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar Es Salaam Machi 21, 2024.

Wajumbe wa Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), wakiongozwa NA Mwenyekiti wake Mhe. Deus Sangu na Menejimenti ya PSSSF wakitembelea jengo la PSSSF Commercial Complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar Es Salaam Machi 21, 2024.

Taswira ya jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex lililoko barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), wametembelea jengo hilo Machi 21, 2024, ili kukagua mradi huo uliogharimu Mfuko wa PSSSF, kiasi cha shilingi Bilioni 232.

Eneo la chini la maegesho ya magari
Majenereta ya usaidizi inapotokea umeme wa TANESCO umekatika
Ngazi za umeme na za kawaida ndani ya jengo la Commecial complex
Bwawa la kuogelea eneo la commercial complex
Mwenyekiti akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati kwenye ghorofa lenye ofisi za UNDP
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakipata maelezo kuhusu wapangaji wa jengo hilo

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), Mhe. Deus Sangu (Katikati), akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul-Razaq Badru huku Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji PSSSF, Bw. Rashid Mtima akishuhudia, wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), kukagua jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar Es Salaam Machi 21, 2024.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), Mhe. Deus Sangu (Katikati), akipeana mikono na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji PSSSF, Bw. Rashid Mtima huku Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul-Razaq Badru, akishuhudia, wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Public Investment Committee-PIC), kukagua jengo la kitega uchumi la PSSSF Commercial Complex barabara ya Sam Nujoma jijini Dar Es Salaam Machi 21, 2024.


Picha ya pamoja


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...