Afisa kilimo wa Chama kikuu cha ushirika wilaya ya Tunduru(Tamcu) Grace Evody,akizungumza katika kikao kazi kati ya wakulima,viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika jana kwa ajili ya mikakati ya kuongeza uzalishaji wa mazao kwa msimu wa kilimo 2023/202

Na Mwandishi wetu, Tunduru

MWENYEKITI wa Chama kikuu cha ushirika wilayani Tunduru(Tamcu Ltd)Mussa Manjaule,amewaagiza maafisa ugani wa chama hicho,kuhakikisha wanakwenda kwa wakulima kutoa elimu ya kilimo cha kisasa itakayosaidia kuongeza uzalishaji mashambani.

Aidha,amewataka wakulima wa zao la korosho,ufuta,mbaazi na mazao mengine yanayouzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kujiunga katika vyama vya msingi vya ushirika ili waweze kupata huduma za ugani kwa urahisi.

Manjaule,ametoa maagizo hayo jana wakati akizungumza na wawakilishi wa wakulima,viongozi wa Amcos na watendaji wa Chama kikuu cha Ushirika(TAMCU LTD)katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa chama hicho.

Katika hatua nyingine,Manjaule amewaonya vijana kuacha kukaa vijiweni na kucheza kamali au pool,badala yake wajikite katika shughuli za uzalishaji mali ikiwemo kilimo cha korosho ili waondokane na umaskini.

Afisa kilimo wa Chama hicho Grace Evody,amewashauri wakulima kutumia mbegu bora zinazostahimii magonjwa na hali ya ukame,badala ya kununua mbegu za mitaani zinazotoa mavuno kidogo.

Kwa upande wake kaimu meneja wa bodi ya korosho Tanzania(TCB) tawi la Tunduru Samwel Kambona alisema,wameaanza kusajili wakulima wote wa korosho kwa lengo la kuwatambua na kupata idadi kamili wanaostahili kupata pembejeo za ruzuku.

Alisema,mpango huo unalenga kurahisisha uendeshaji wa zao la korosho,kupata idadi ya pembejeo zinazohitaji na wakulima wa zao hilo ili kuepusha vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa Amcos.

Pia alisema kuwa,mango huo utaisaidia bodi ya korosho kuwa na takwimu sahihi za wakulima,idadi ya mikorosho ili kurahisisha utoaji wa huduma za ugani kwa wakulima.

Alisema,taarifa hizo zitatumika katika zoezi zima la ugawaji wa pembejeo ili kuwaondolea wakulima changamoto ya upatikanaji wa pembejeo wanapoanza maandalizi ya uzalishaji wa zao hilo.

Kambona,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kutoa ruzuku ya asilimia 100 kwa wakulima wa korosho na kusisitiza kuwa,nje ya mfumo huo hakuna mkulima atakayepata viautilifu vya ruzuku badala yake watalazimika kununua kwa wafanyabiashara, .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...