Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ameanza ujenzi wa viwanja vya michezo ya mpira wa kikapu(basketball),mpira wa pete(netball) na mpira wa wavu(volleyball) katika eneo la shule ya Sekondar Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma.

Ujenzi huu unatokana na ahadi ambayo Mbunge Mavunde aliitoa wakati wa mahafali ya wanafunzi wa kidato cha IV alipokuwa Mgeni Rasmi.

Akizungumza na wanafunzi leo asubuhi alipiwatembelea shuleni,Mbunge Mavunde amesema kiwanja hicho ambacho kitatumika kwa matumizi ya aina tatu ya michezo kitakuwa ni cha kisasa na kitasaidia kukuza michezo na vipaji vya wanafunzi wa Dodoma Jiji.

Pamoja na ujenzi huo,Mbunge Mavunde ameahidi kuweka taa katika uwanja huo ili uwe unatumika muda wote,kugawa seti za michezo na kununua tanki la kuhifadhi maji.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya shule,Mkuu wa Shule Sekondari Kiwanja cha Ndege Ndg. Daniel ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa madarasa na fedha Tsh 50,000,000 za umaliziaji ujenzi wa maabara na kuongeza pia kukamilika kwa ujenzi wa michezo hapo shuleni utasaidia kuimarisha afya za wanafunzi na kukuza vipaji vyao kupitia michezo.

Akitoa shukrani zake,Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege Mh. Amos Mbalanga amemshukuru Mbunge Mavunde kwa ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya kuimarisha michezo na kuahidi kusimamia ujenzi wake kukamilika kwa wakati.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...